Kushuka Kwa Thamani ya Shilingi

Sundi

Member
Jun 21, 2011
90
33
Wadau, ninaomba msaada kuhusu maswali mawili :

- Kwanini thamani ya shilingi inashuka wakati bei ya dhahabu inapanda kwa kasi kwenye soko la dunia

- Serikali ina mkakati wowote unaodhibiti hali hii inayosababisha bidhaa zote zinazoagizwa hasa mafuta kupanda kila wakati kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi..
 
Mkuu nchi haina mipango, kushuka kwa shilingi hakuna anayeshtukia isipokuwa imegeuzwa dili. Fikiria tu jinsi soko holela lilivyo na nguvu kuliko serikali, fikiria pia upuuzi unaofanywa kama kuchapisha pesa harafu zinapotea kimaajabu (refer in january 2011). Kifupi serikali inaposhindwa kuona hata hii hali basi ujue serikali yetu ipo mfukoni mwa mataifa makubwa na wafanyabiashara wakubwa nk.
 
Kwani tuna hata hiyo unayoiita dhahabu hapa?
Hakuna kitu hapa ndugu yangu, na kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu, uchumi wetu uko huria kwa wafanyabiashara wachache wenye influence hadi BOT.
 
Kwani tuna hata hiyo unayoiita dhahabu hapa?
Hakuna kitu hapa ndugu yangu, na kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu, uchumi wetu uko huria kwa wafanyabiashara wachache wenye influence hadi BOT.

Big up! Nakubaliana na wewe mkuu! Thanks
 
Kuna tatizo jingine la kupenda sana kutumia washauri waelekezi kutoka nje ambao mara nyingi tunalazimishwa na wafadhili ili kufanya fedha zao ambazo huzileta huku kwa jina la misaada ziweze kurudi kwao na kutoa ajira kwa watu wao. mara nyingi (kama sio zote) washauri hawa hutoa mapendekezo ambayo yatazisaidia nchi zao na kutuacha sisi tegemezi. hii ni moja ya sababu hatuna sera nzuri za fedha na shilingi yetu kushuka kila uchapo.
 
Back
Top Bottom