Wa nyamadyaki
JF-Expert Member
- Mar 6, 2013
- 1,178
- 529
Nashukuru Mkuu kwa kuja na taarifa mrejesho (feedback) ya nauli kushushwa.Leo nimepanda daladala kutoka ninakoishi ambapo kwa kawaida huwa tunatozwa nauli ya 500 lakini leo nimetozwa 450 na baada ya kuliza na kufanya kautafiti kadogo nikaambiwa kwamba nauli imeshushwa jijini dar kuanzia leo,
Wana JF wenye taarifa sahihi tafadhar
heeee nauli ya daladala ndio nini?
Bangi hizi...heeee nauli ya daladala ndio nini?
heeee nauli ya daladala ndio nini?
Nashukuru Mkuu kwa kuja na taarifa mrejesho (feedback) ya nauli kushushwa.
Juzi kuna thread ililetwa hapa jamvini kuhusu UKATISHWAJI WA RUTI n.k.
Watu wenye dhamana na kazi zao wako makini na matatizo ya wananchi yatashughulikiwa kupitia vyombo husika. Tuwe wepesi kutoa taarifa kwenye vyombo husika na hapa Jamvini.
Walichokuwa wanafanya hawa Makondakta na Madereva ni wizi ..na Hilo suala limeanza kushughulikiwa na mamlaka husika.
Watanzania TUAMKE na kuanza kutoa ripoti kuhusu Uhujumu uchumi kuanzia ngazi za chini...tusilalamike tu Serikali haifanyi kazi. Tuisaidie Serikali na vyombo husika kutekeleza na kuwanyoosha wavunja sheria. PAMOJA TUNAWEZA.
na pantoni si kama daladala?Sijapanda daladala mda mrefu so sijui nauli halisi...je hyo 450 kutoka wapi hadi wapi? Nauli kawaida ni sh 400.
Leo nimepanda daladala kutoka ninakoishi ambapo kwa kawaida huwa tunatozwa nauli ya 500 lakini leo nimetozwa 450 na baada ya kuliza na kufanya kautafiti kadogo nikaambiwa kwamba nauli imeshushwa jijini dar kuanzia leo, Wana JF wenye taarifa sahihi tafadhar
Nauli haijashushwa bali inawezekana ulikuwa unaibiwa tena mchana kweupe.
Kwa kawaida nauli Dar zilitakiwa kuwa, 400, 450, 600, na 750 kulingana na umbali wa safari.
Inaonekana badala ya kutozwa 400 au 450 ulikuwa unatozwa 500 halafu ukaona ni sawa tuu.
Tatizo bongo watu wakiibiwa wala hawajiulizi. Ndiyo maana ikaitwa Bongo tambarare.
Bongo unakula utakavyo maana wenye jiji don't give a damn really.
Ukiwapa haki yao watakushukuru ile mbaya na kukuona kama umeshuka mbinguni vile.
Tatizo la hii nchi siyo viongozi wake, bali ni wananchi wake. Rahisi sana kuwaibia.
mwaibula yuko wapi?
Dah! Leo ndo mumeniamsha kiukweli nilikuwa naibiwa dah!