Kulikuwa na mkuu wa shule ya sekondari moja ya mchanganyiko hapa nchini jina lake Kačhupillo (jina si halisi). Mkuu huyu aliiongoza shule ile kwa miaka 3 tangu nikiwa kidato cha 1 mpk cha 3. Ktk uongozi wake mwalimu huyu mkuu aliacha kila jambo bora liende.
Walimu walikuwa wakiwachangisha fedha wanafunzi ili wafundishe tuition lkn kwenye vipindi vyao vilivyo kwenye ratiba ya shule wakawa hawaingii. Mwalimu Kachupillo akawa hajali wala hakemei.
Wanafunzi walifanya ufsika watakavyo, na walivuta bangi watakavyo nidhamu na taaluma vikashuka kwa kiwango cha hali ya juu. Mwalimu Kachupillo hakujali.Vyote hivi alichukulia poa.
Ilifika hatua watoto wengi wa kike wakapata mimba, watoto wengi wakaharibika akili kwasabb ya bangi na matukio ya wanafunzi kupigana na kujeruhiana kwa kiwango cha kutisha yakashamiri.
Mwisho wa yote mkuu huyu wa shule alihamishwa. Tukaambiwa anapelekwa wizarani.
Tukaletewa mkuu mpya wa shule. Huyu alikuwa mfuata sheria na taratibu wenyewe humuita 'strict'. Aliwabana wanafunzi na walimu kwa ratiba, na alikataza aina yoyote ile ya mkao au kusimama kati ya mvulana na msichana nje ya darasa.
Mwalimu au mwanafunzi aliyeenda kinyume kidogo tu na taratibu na sheria za shule aliondolewa shule (mwalimu) au alifukuzwa shule (mwanafunzi).
Kuna walimu walijaribu kusuka njama za kuandaa vurugu za wanafunzi ili mwalimu huyu mkuu mpya aonekane hafai lkn kila walipobainika walitimuliwa.
Baada ya kama mwaka hivi mwalimu Kachupillo alikuja pale shule alimsindikiza mwanaye ambaye alikuwa amechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ktk hiyo shule. Walimu na wanafunzi walipomuona walilipuka kwa shangwe na nderemo wakiimba tumekumisi.
Walimu wamemiss biashara zao tuition na kutoroka vipindi vya darasani na wanafunzi wamemiss bangi na uhuru wa kufanya ufuska. Wamemiss maovu.
JK hakuwa tofauti sana na Mwalimu Kachupillo. Aliacha kila mtu afanye yake.
=Wenye kujaza wafanyakazi hewa
=Wenye kutengeneza escrow
=Wabunge kuzoa posho sita kwa siku
=Wabunge kufanya ziara za mafunzo nje ya nchi zisizo na tija
=Bodi za mashirika kufanya mikutano yap nje ya nchi
=Wauza unga kuuza na kuusafirisha waziwazi
=seminar na makongamano yasiyo na tija kufanyika holela
=Kubadili ofisi za umma kuwa sehemu za upigaji
N. K
Haya maovu ndiyo wabunge wameyamiss maana yaliwanufaisha.
Nani asiyejua kuwa kandarasi nyingi za halimashauri zilishikwa na wabunge?
JPM ni strict ndiyo maana mnammiss Kachupillo.