Kusema kweli maisha ni magumu

Kusema kweli maisha ni magumu

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
276
Reaction score
1,428
Kwa wale mliopo mjini mnaweza msijue mateso waliyonayo wa kijijini ila maisha haya wanayoishi siyo Yale waliyoahidiwa.

Piga gharama anayotumia mkulima kuzalisha alafu angalia bei ya soko, mahindi gunia elfu arobaini alafu mfuko mmoja wa cement elfu ishirini je huyu mkulima atajenga? Ada ya mwanafunzi chuo si chini ya milioni, je utauza magunia mangapi mtoto asome?

Hapo ni mfano zao moja, ila wakulima wa mbaazi, korosho, kahawa, pamba na alizeti nao wanalia njaa Bei si nzuri.

Wafanyakazi nao kipato Chao ni kilekile toka mwaka 2014 hadi leo na Hawa ndio waliokuwa Wanashamirisha biashara lakini siku hizi wanaishi kwa kuweka daftari kwa mangi walipe mwisho wa mwezi

Waajiri binafsi nao wamefunga biashara si kwamba Tanzania hakuna biashara Bali ni kwa sababu wenye fedha za kununua hawapo lakini pia Sera yetu ya uwekezaji si rafiki kwa wawekezaji.

Waliokuwa wana ajira wanazipoteza na waliokuwa hawana ajira ndo hivyo tena hawaajiriwi.

Kuhusu ujasiriamali, watu wengi walijikita kwenye ufugaji ukiwemo ufugaji wa kuku, wanasiasa bila utafiti wakawafukuza wale waliokuwa wanaleta vifarana na baadhi ya virutubishi kutoka nje zikiwemo mashine kwa kisingizio Cha kulinda wajasiriamali wa ndani muda si muda biashara hiyo imedorora na tunaanza Tena kushawishi wale tuliowafukuza wake tena kuwekeza.

Tunapiga Vita ya umaskini kwa kuongeza maskini kila siku badala ya kupunguza hao maskini
 
Our president has tried but his policies has never put back people to work/unemployment rate is so high
 
Our president has tried but his policies has never put back people to work/unemployment rate is so high
Wengi hawatakuelewa, Lumumba buku 3 watakuja utadhani wao wanalishwa na Polepole, hali imekua ngumu sana tuacheni utani.
Yaani kuna wehu huwa wanatetea ujinga wa serikali utadhani ni mawakili wa serikali au yeye anaishi USA.These marabooks should go to hell!!
Yan I mimi si usiku si mchana usingizi hauji kabisa, hali tete kila kukicha
 
Inauma sana hasa kwa sisi vijana ambao tumeanza Maisha awamu ya huyu jamaaa... yani chenga tupu na hatuoni hata matumaini huko mbele
 
Back
Top Bottom