Kusajili laini za simu kutumia alama za vidole

Kusajili laini za simu kutumia alama za vidole

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Taarifa za hivi karibuni zilitolewa na TCRA kuwa kila Mwananchi aliye na simu aisajile simu/zake kwa kutumia vidole na sharti awe na kitambulisho cha Taifa kilichotolewa na NIDA. kwa siku za karibuni kulitolewa taarifa kuwa kati ya watu millioni kumi na tisa waliojiandikisha ni watu millioni nne na nusu ndiyo tayari wamekwishapata vitambulisho vya Kitaifa. Mimi binafsi niliandikishwa Januari, 2018 na mpaka leo sijapata kitambulisho. Pamoja na Mhe. Rais kuwashauri NIDA kujitahidi kuwa watu wote waliojiandikisha wawe wamepata vitambulisho sidhani kuwa kufikia Desemba Wananchi wote waliojiandikisha wanaweza wakapata vitambulisho. Mimi sina kitambulisho nitajisajili vipi na lini pamoja na kuwa Mhe. Rais ametoa ufafanuzi juu ya suala hili. Kuna sehemu nilisoma kuwa Mkandarasi tayari amemwaga manyanga sijui ni kweli?. Tunaiomba NIDA ifanye haraka ili kila Mwananchi apate kitambulisho cha Taifa.
 
Serikali yenu tukufu inafanya kila linalowezekana kuhakikisha kila raia anakuwa na Kitambulisho chake.
 
Kashasema, zoezi la kusajili line liende sambamba na utolewaji wa vitambulisho vya taifa...

Kwa sababu siyo wote ambao tayari wamevipata...

Kwa hiyo ondoeni shaka...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom