Kusaga ampigia simu Diamond Platnumz akiwa live Clouds FM

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,043
Kusaga alikuwa live anawapigia simu watu na mashirika mbalimbali watoe michango yao kwa ajili ya mapambano ya corona, akampgia Diamond.

Diamond kakubali kuchangia ila kasema mchango wake utatajwa kesho. Kusaga kamwambia ataje wimbo wake ambao upigwe, akachagua sitobaki kama nilivyo wa joel luhagwa.

Akamsisitiza achague wa kwake, akajibu nina nyimbo nyingi nyie chagueni wowote mnaotaka.

Kusaga amsisitiza jamaa kagoma mwisho kasema au pigeni wimbo nilioshirikishwa.

Naona Mond hataki tena nyimbo zake zipigwe Mawingu.
 
Huyu anayepigia watu live wachangie hafai. Huko ni kuwaharibia kabisa ni kama kawalazimisha sababu ukiwa live Tanzania nzima inakusikia ni ngumu kukataa utaonekana mbaya. Sema hajakutana na watu kama mimi, unanipigia live nakukatia simu sipendi ujinga.

Diamond ashasema anatoa msaada kwa watu 50k sijui 500k wenye maisha ya chini. Bado wanazidi kumkaba, kama anataka kusaidia muacheni atasaidia akijisikia
 
Hahaha, mtu unaweza kujiharibia siku bure kwa kuwashtukiza watu.

Diamond ni media owner kwa sasa, wewe kutangaza kupitia media nyingine na kutaka yeye achangie ili media hiyo ipate credit kwamba imewachangisha watu si kitu sahihi.

Yeye alitakiwa kuwapigia business partners wa Clouds, na kama anataka angeenda Wasafi kufanya utaratibu kama huo na kuwapigia watu anaoona ni business partners wa Wasafi.
 
Hayo yalitokea asubuhi ya leo wakati Clouds Media wanafanya kipindi chao cha Power Breakfast ambapo walimuunganisha kusaga ili achagize kampeni ya kuwachangia wahudumu wa afya kukabiliana na janga la corona.

MD kusaga aliwapigia simu marafiki zake kibiashara ili waweze kuchangia kampeni hiyo ambapo miongoni mwa watu aliowapigia alikua msanii Nasib Abdul (Diamond).

Ikumbukwe kwa miaka mingi kituo cha Clouds hakijihusishi kwa lolote na msanii Diamond na hata kulitaja jina lake imekua ni sumu ndani ya kituo hiki

Katika hali ambayo inaonekana kama wameshtukizwa na bosi wao, watangazaji hao wa Clouds ambao ni Siza na Babra Hassan waliongea na Mondi kwa kigugumizi cha hali ya juu sana hasa pale Kusaga alipowaambia wamuulize Mondi anataka wapige nyimbo gani kutoka kwake

Diamond Platnumz kwa upande wake aliongea kwa upole na kujiamini kwa hali ya juu ila alikataa kutaja ni nyimbo gani anataka ipigwe kituoni hapo.

Aliwaambia pigeni yoyote mnayoipenda

Source: Power Breakfast, Clouds radio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni taarifa ama udaku au breaking news au nipashe ama isiyo najina..??
 
Kusaga ni Vyema Awaachie Vijana Waendeshe Kampuni hana analolijua, Vijana wa Pale mjengoni hawataki kumsikia Diamond na Diamond hataki Kuisikia Clouds, kusaga awaache kila mtu aendelee ni mishe zake Uwezo Wake ni Mdogo kwa kua ni Boss bas anataka Kuforce Vitu visivyowezekana, Ruge alimbeba sana huyu Kusaga

Kipindi kile alijipendekeza akawaamlisha vijana wapige Nyimbo za Diamond, Mameneja wake wakamshushua, Bado anangangania tu aache Upimbi na Kujipendekeza kwa Diamond,.
 
Back
Top Bottom