Kusafisha tumbo msaada

Fuata ushauri utafanikiwa. Ukikwama weka mawasiliano tukutafute na kukupa ushauri zaidi.
 
nenda aiusha utapewa dawa ya kuarisha siku nzima bada ya hapo unakula kisusio unarud kuwa kama mtoto mpyaa
 
Matunda yafuatayo yanasaidia kusafisha sumu mwilini:
1. Mapapai
2. Mananasi
3. Maembe

Utumiaji:
Unatakiwa kula moja ya matunda hayo kwa siku tatu mfululizo bila kula chakula kingine chochote. Zaidi unatakiwa unywe maji mengi pia. Ulaji huo wa matunda ni kwa ule muda wa kula chakula yaani asubuhi, mchana na usiku.

Hali isiyo ya kawaida:
1. Utakwenda haja kubwa zaidi ya mara kwa mara tena choo chepesi
2. Njaa itakusumbua kwa kuwa tumbo halijazoea kula matunda tu kwa siku
Hili zoezi linatakiwa lirudiwe kila baada ya miezi mitatu.
 
Asanteni sana kwa ushauri wenu. Ila nimekuwa natafuta mlonge sijafanikiwa kama kuna mtu anajua mahali ulipo tafadhari nijulishe
 



Unavutia biashara nini?
 
jamani huo mlonge unapatikana wapi....? una jina lingine....?
 
Hapa ni JF kila mtu ana lake na ana haki ya kulisema kama ni biashara haya ,kama ni utani haya kukusaidia kuna dawa za asili ambazo zilitumika tangu enzi za mababu kusafisha tumbo,ambamo faida zake ni pamoja na kupunguza nyongo,ngiri ya kiume na kike na kupunguza matumbo (utando matumbo) usio na kazi ndani ya mwili wa binaadam
kama upo arusha karibu uipate kuna Haruna ,pia dar zipo kwa wamasai kama hawatachakachua ni automatically kwenye kijiko kidogo cha chai na huisha pale nyongo inapoisha
 
Jamani nasikia kuna njia za kusafisha tumbo . Yaani binadamu anatakiwa kusafisha tumbo kwa kutoa sumu mwilini , uchafu n.k
kama kuna mtu ana idea juu ya hilo naomba kujuzwa

I know someone who can assist with fresh foods.
He mixes fresh fruits, vegs, and some spices, blends them to liquid form, no water added.
Unakunywa 3 times a day. Ila mchanganyiko unakuwa na onions, ginger, garlic, limao, apples, apricots,
etc. Vitunguu vinaleta ugumu wa kuinywa ila ukiwa na nia unakunywa. Kisha pia ana unga wa uji, ugali, atapenda uache
kula nyama, samaki etc. Atakushauri ule vegs, legumes, fruits.
All these helps to cleanse the body, si tumbo peke yake. Ila yuko expensive the liquid mixture has it's price, unga wa uji, ugali etc pia bei yake tofauti haviendi na the liquid drink. Are you interested?
 
Jamani nasikia kuna njia za kusafisha tumbo . Yaani binadamu anatakiwa kusafisha tumbo kwa kutoa sumu mwilini , uchafu n.k
kama kuna mtu ana idea juu ya hilo naomba kujuzwa

mkuu unazifahamu kazi zote za maji mwilini?. basi kabla ya kuanza dawa yeyote pitia usome kwanza kazi za maji mwilini hapa: http://maajabuyamaji2.artisteer.net/kwanini-unahitaji-maji-kila-siku/ halafu utamua kama uende dukani kununua dawa leo leo au utasomasoma notisi hizo.
 
Jamani nasikia kuna njia za kusafisha tumbo . Yaani binadamu anatakiwa kusafisha tumbo kwa kutoa sumu mwilini , uchafu n.k
kama kuna mtu ana idea juu ya hilo naomba kujuzwa

Bila chenga yeyote maji husafisha tumbo kirahisi kama kumsukuma mlevi vile, tuone kazi za maji mwilini:

‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa – dr. Batmanghelidj'.

Baada ya oksijeni, maji ndicho kitu pekee ili kuishi. Chini utasoma baadhi ya sababu 41 za umhimu wa maji mwilini:



  • Bila maji hakuna kinachoishi. Wakati wowote unapopungukiwa maji, seli zako hufa.

  • Panapotokea upungufu wa maji, kitu kimoja lazima kipotee, baadhi ya kazi za seli hufa.

  • Maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu, maji ndiyo hela ya mwili, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

  • Maji hutumika kama moja ya malighafi katika usanifu na ujenzi wa seli, huziweka seli pamoja.

  • Maji hukinga uharibifu wa vinasaba (DNA), Vinasaba vichache visivyo vya kawaida huzarishwa.

  • Maji kwa uwezo mkubwa yanaongeza uwezo, nguvu na kinga ya mwili, ujuzi huu wote unahusisha pia dhidi ya kansa.

  • Maji ni wakala mhimu katika mmeng'enyo wa vyakula karibu vyote, vitamini na madini.

  • Maji yanatumika kusafirisha vitu vyote mwilini, maji yanapoifikia seli, huipa pia oksijeni na kuchukuwa hewa chafu hadi kwenye mapafu ili kutolewa nje ya mwili.

  • Maji huzisomba taka chafu toka sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye Ini na Figo ili kutolewa nje.

  • Maji ni mhimu ili kulainisha sehemu zote za mwili, hivyo kuzuia kufunga choo.

  • Maji huzuia shambulio la moyo na mshituko.

  • Maji ni mhimu katika kuupooza na kuupa mwili joto.

  • Nguvu za kiumeme katika maji hutupa nguvu za kufikiri, kufikiri kunahitaji nguvu, hivyo kuhitaji maji.

  • Maji ndicho kiamusho au kichangamusho (pick-me-up) pekee bora cha miili yetu kuliko kinywaji kingine chochote duniani, bila madhara.

  • Maji yatakurudishia usingizi wa kawaida na mororo, kila tuotapo ndoto mbaya au za kutisha (nightmares), mwili huwa unatuamusha kwenda kunywa maji. jaribu hii, siku yeyote ukiota ndoto ya kutisha, amka na kunywa glasi moja ya maji kisha rudi kulala.

  • Maji huzuia uchovu, huwapa vijana nguvu. Fikiri: unapokuwa na uchovu na ukaamua kuoga, baada ya kuoga sehemu kubwa ya uchovu hupotea. Hapo umeoga tu, je ukiyanywa maji yenyewe?!!.

  • Maji hutengeneza ngozi nyororo hivyo kuzuia kuzeeka mapema.

  • Maji yatausawazisha katika hali yake ya kawaida mfumo wa uzarishaji damu kwenye mifupa, hivyo kuzuia Leukemia na Anaemia.

  • Maji yatapunguza maumivu ya ishara za kutokea kwa hedhi.

  • Upungufu wa maji mwilini huzuia uzarishwaji wa homoni za kiume na kike, hii ndiyo sababu ya kwanza ya uhanithi (impotence) na kukosa hamu ya tendo la ndoa (negative sex libido).

  • Kunywa maji kutakutofautishia hisia za njaa na kiu ya maji, kunywa maji kwa muda na upunguze uzito na unene bila kuacha kula (dieting).

  • Maji yatazuia homa za asubuhi kwa mama mjamzito.

  • Maji yataunganisha mawazo na kazi za mwili, yataongeza uwezo katika kutambua malengo na nia.

  • Maji yatageuza utegemezi kwa vilevi ikiwa ni pamoja na pombe, kafeina na baadhi ya madawa ya kulevya.

  • Maji huzarisha nguvu za kiumeme na nguvu za kisumaku katika kila seli ya mwili - nguvu za kuishi. Nguvu za kiumeme zinafanya kazi kama nguvu za kisumaku na kuvipanga vitu anuwai kama sumaku hivyo kutoa uwepo wake sahihi na kujihusisha na matendo ya kikemikali.

  • Maji yanatumika katika kuvikatakata vyakula kuwa vipande vidogovidogo na hatimaye umetaboli wake.

  • Maji yatakiongezea nguvu chakula (transfoma chocheo ya chakula) na hatimaye chakula kutoa nguvu kwa mwili wakati wa umeng'enywaji wake.


  • Maji yataongeza uchukuwaji wa viini lishe mhimu vilivyomo kwenye chakula.

  • Maji ni kilainishi kikuu kwenye maeneo ya maungio (joints) na hivyo kuzuia ugonjwa wa yabisi na kupooza.

  • Maji hutumika kwenye 'diski' za uti wa mgongo kuzifanya zigongane na kufyonza maji.

  • Maji huzuia kuzibika (clogging) kwa ateri kwenye moyo.

  • Maji huzuia kupunguwa kwa umakini na usikivu kwa watoto na watu wazima (Attention deficit disorder - ADD).

  • Maji huongeza ufanisi katika kazi.

  • Maji yatazuia mfadhaiko, pupa na kukata tamaa.

  • Maji huzuia ugonjwa wa Glakoma.

  • Maji yataiyeyusha damu na kuizuia isigande wakati wa mzunguko wake.

  • Upungufu wa maji unavihifadhi vijidudu nyemelezi (free radicals) mwilini, na maji ndiye muondoaji mkuu wa vijidudu hivi nyemelezi.
  • Maji hutoa nuru na mng'aro kwa macho na kuhimili kuona kwa sababu kushughulika na taarifa za mwanga kunahitaji nguvu nyingi katika kusafirisha taarifa toka mfumo mmoja katika jicho kwenda katika mfumo mwingine kwenye ubongo ili kutafusiriwa.

  • Maji na mapigo ya moyo vinatengeneza muyeyuko na mawimbi ili kuzuia vitu visivyotakiwa kubaki kwenye mkondo wa damu.

  • Mwili wa binadamu hauna hifadhi (store) ya maji, ndiyo maana unatakiwa kuyanywa kila siku.

  • Kunywa maji halisi, safi na salama kwa kanuni sahihi, kunausafisha mwili, maji yanaiacha sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (colon) kuwa na uwezo zaidi wa kutengeneza damu mpya (fresh blood) ijulikanayo katika lugha ya kitaalamu kama 'Haematopaises', kwamba difu la utumbo mkubwa na utumbo mdogo (mucousal fold) huamushwa upya kwa njia hii.

Ifike mahala tuache mazoea ya kuipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).

"kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo, kwenda shule hutusaidia tu, japo hatuwezi kwenda shule, twaweza kujielimisha – Mwl.J.k.Nyerere".

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.

www.maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Sasa si unatengeneza bom tumboni? colleague watakupanga jina...
 

Mwili wa binadamu una mifumo yote ya kutolea sumu kama figo maini n.k. Kwa hiyo hauhitaji external artificial assistance. Unaweza kukwangua utumbo ukasababisha vidonda.
 
Pia unaweza kusafisha tumbo bila kutumia dawa,
Chemsha maji na uyanywe yakiwa moto yasiyochanganywa chochote siku nzima
Pia usile chochote ni maji moto tu siku nzima hapo utakuwa umelisafisha tumbo lako
 
Vipi kuhusu ENEMA wakuu nani anajua juu ya hiyo njia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…