ndugu inategemea hiyo gari imelipiwa sh. ngapi zenji, imeingia lini zenj. mfano gari iliyoingia zenj mwaka juzi ushuru wake unakua mdogo kulinganisha na iloingia mwaka huu. Pia kina kitu tofauti yaani kama gari inatakiwa ilipiwe mil 5 na zenj ikalipiwa Mil 2 manaake hizi 3 lazima ukazilipe bara. ww una gari gani kwani? limeingia lini na ushuru limelipiwa bei gani zenj?
Heshima kwenu,
Naomba kujua kwa wale waliowahi kusafirisha gari toka Zanzibar ambayo imelipiwa kila kitu na imesajiliwa kwa namba za ZNZ inahitajika kulipia TRA?
Kiasi gani kwa gari isiyozidi 2000cc?
Tafadhali naomba kujua
Gharama kubwa ni kuisafirisha...kama unatumia agent wa z'bar kuisafirisha na kuiclear bandarini dar, ww anakuletea unaanza kuendesha ikiwa tayari na namba za bara ni kama tzs 1m hivi. Ila gharama kubwa ni usafiri wa meli.
Mzoefu aje afunguke zaidi,