Kurusha Jini Kumerudi?

Kurusha Jini Kumerudi?

Nkamu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Posts
227
Reaction score
91
Salama wakuu?

Juzi nilikuwa nasafiri kutoka Mbeya kwenda Dar kwa gari ndogo. Tulipofika Mbuyuni wilaya ya Rujewa, tulisimamishwa na askari wa usalama barabarani. Baada ya kusimama askari akaomba leseni ya dereva. Baada ya kuchukua leseni dereva akaambiwa anaadhibiwa kwa kuendesha gari kwa spidi kubwa kuliko 50kph. Dereva alipojitetea kwamba sio kweli, alioneshwa picha kwenye simu ya askari ambayo ametumiwa na askari mwingine ambaye alikuwa Chimala na kamera ya spidi - karishiwa jini na mwenzie aliye mbali na mahali walipokamata hilo gari.

Ninachokumbuka ni kwamba wakati wa Waziri Kangi Lugola, mchezo huo ulipigwa marufuku. Sasa je, maagizo yote yaliyotolewa na waziri anayeondoka madarakani yanakoma mara baada ya uteuzi kukoma? Au tulionewa na yule askari?

Naomba kuwasilisha.
 
Wanajamii mbona kimya? Au hili tatizo haliwahusu?
 
Nchi hii haina kanuni za kudumu inaongozwa kwa matamshi ya viongozi majukwaani. Watanzania tusifanye makosa October.
 
Tukujibu nini na wewe Uzi wako ni wa kinyanyapaa
 
Back
Top Bottom