Kurunzi ya kisiasa: Jinsi CHADEMA inavyopwaya na kushindwa kwenda na kasi ya mh Magufuli na CCM mpya

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
539
642
Na
Augustine Chiwinga.

Ni ukweli ulio wazi kwamba chama cha CHADEMA kimeshindwa kwenda na kasi ya Mh Rais Magufuli anayeongoza serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kwa sasa kinajifanyia mageuzi makubwa chini ya kauli mbiu ya "CCM MPYA NA TANZANIA MPYA."

Mojawapo ya mageuzi makubwa inayoyafanya CCM ni kuisimamia serikali kikamilifu kutimiza wajibu wake kwa wananchi pamoja na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015 -2020 ambayo pamoja na mambo mengine imeagiza kupambana kufa na kupona na vitendo vya rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya ,nidhamu kwa watumishi wa umma , ujambazi na kila aina ya uovu ulioota mizizi ndani ya nchi yetu.

Kutokana na kasi kubwa ya kiutendaji ya Rais Mh Dr John Pombe Magufuli chini ya mageuzi ya CCM mpya chama cha CHADEMA kimejikuta kimeachwa nyuma kwenye kasi hiyo hivyo kimegeuka kua chama cha kutetea uovu na waovu wazi wazi bila ya kupepesa macho wala aibu,huku nakuita ni kupwaya kisiasa.
Ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga vita ya madawa ya kulevya? , ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga kufukuzwa kazi kwa mafisadi serikalini ? ni nani alitegemea leo CHADEMA kutetea majambazi? ni nani alitegemea Leo CHADEMA kutetea raia wa kigeni wasio na sifa kujazana katika makampuni na mahotel hivyo kunyima vijana wetu fursa za ajira ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga uanzishwaji wa mahakama maalumu ya mafisadi.?

CHADEMA kimepwaya kimebaki kua ni chama cha kutoa matamko ya uchochezi na kuchonganisha wananchi na serikali.
Kimebaki kua chama cha wapika majungu uzushi na waongo kisichokua na hoja ,maono wala dira na kwa mwendo kinaoenda nao ni wazi kwamba kinajichimbia kaburi lake taratibu na kwa kuthibitisha hilo ni matokeo ya uchaguzi mdogo uliopita ambapo kiliangukia pua.

Wananchi wa Tanzania wanashukuru wamepata Rais anayeshughulika na matatizo ya watu na kuyapatia ufumbuzi kwa haraka, akitekeleza vilio vyao vya muda mrefu kwa umakini mkubwa chini ya usimamizi wa CCM mpya.

Leo CHADEMA imefikia hadi ya hatua ya kuhariri (Edit) video ili kumuonesha Rais Magufuli hakumpa nafasi mkalimani wake katika kuongea kule Addis Ababa huku ni kupwaya na uchakavu wa kisiasa.Nafikiria kusema kwamba CHADEMA mwisho wao umefika nao wataungana kwenda kuzimu na vyama vingine vilivyokuja kwa kasi kubwa kama vile NCCR-MAGEUZI.
CHADEMA hawakujiandaa kwenda na kasi ya Mh Magufuli wao walidhania mambo yatakua kama kama walivyozoea ( Business as usual) kumbe sivyo wameachwa nyuma na tayari wameshapwaya kisiasa , kapatikana mtu ambaye amedhamiria kulinyoosha taifa mwenye kuzijua shida za watanzania nkul
Augustine Chiwinga.

Ni ukweli ulio wazi kwamba chama cha CHADEMA kimeshindwa kwenda na kasi ya Mh Rais Magufuli anayeongoza serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kwa sasa kinajifanyia mageuzi makubwa chini ya kauli mbiu ya "CCM MPYA NA TANZANIA MPYA."

Mojawapo ya mageuzi makubwa inayoyafanya CCM ni kuisimamia serikali kikamilifu kutimiza wajibu wake kwa wananchi pamoja na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015 -2020 ambayo pamoja na mambo mengine imeagiza kupambana kufa na kupona na vitendo vya rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya ,nidhamu kwa watumishi wa umma , ujambazi na kila aina ya uovu ulioota mizizi ndani ya nchi yetu.

Kutokana na kasi kubwa ya kiutendaji ya Rais Mh Dr John Pombe Magufuli chini ya mageuzi ya CCM mpya chama cha CHADEMA kimejikuta kimeachwa nyuma kwenye kasi hiyo hivyo kimegeuka kua chama cha kutetea uovu na waovu wazi wazi bila ya kupepesa macho wala aibu,huku nakuita ni kupwaya kisiasa.
Ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga vita ya madawa ya kulevya? , ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga kufukuzwa kazi kwa mafisadi serikalini ? ni nani alitegemea leo CHADEMA kutetea majambazi? ni nani alitegemea Leo CHADEMA kutetea raia wa kigeni wasio na sifa kujazana katika makampuni na mahotel hivyo kunyima vijana wetu fursa za ajira ni nani alitegemea leo CHADEMA kupinga uanzishwaji wa mahakama maalumu ya mafisadi.?

CHADEMA kimepwaya kimebaki kua ni chama cha kutoa matamko ya uchochezi na kuchonganisha wananchi na serikali.
Kimebaki kua chama cha wapika majungu uzushi na waongo kisichokua na hoja ,maono wala dira na kwa mwendo kinaoenda nao ni wazi kwamba kinajichimbia kaburi lake taratibu na kwa kuthibitisha hilo ni matokeo ya uchaguzi mdogo uliopita ambapo kiliangukia pua.

Wananchi wa Tanzania wanashukuru wamepata Rais anayeshughulika na matatizo ya watu na kuyapatia ufumbuzi kwa haraka, akitekeleza vilio vyao vya muda mrefu kwa umakini mkubwa chini ya usimamizi wa CCM mpya.

Leo CHADEMA imefikia hadi ya hatua ya kuhariri (Edit) video ili kumuonesha Rais Magufuli hakumpa nafasi mkalimani wake katika kuongea kule Addis Ababa huku ni kupwaya na uchakavu wa kisiasa.Nafikiria kusema kwamba CHADEMA mwisho wao umefika nao wataungana kwenda kuzimu na vyama vingine vilivyokuja kwa kasi kubwa kama vile NCCR-MAGEUZI.
CHADEMA hawakujiandaa kwenda na kasi ya Mh Magufuli wao walidhania mambo yatakua kama kama walivyozoea ( Business as usual) kumbe sivyo wameachwa nyuma na tayari wameshapwaya kisiasa , kapatikana mtu ambaye amedhamiria kulinyoosha taifa mwenye kuzijua shida za watanzania na kulivusha taifa kutoka mahali lilipoganda kwa muda mrefu hadi sehemu nzuri kwa maslahi ya watu wote wa Tanzania na tayari ameshaanza kutenda.
Chadema kimejipa kazi ya kupaka rangi dhambi na kubadilisha batili kua halali na kwa hakika mwisho wao umekaribia.

Augustine Chiwinga
 
Ujinga ni tunu ya bure. Umejaliwa au amejaliwa kutumia kalamu yake kuendeleza hoja ya kijinga.

Ila ndiyo inayowangizia siku.
 
Sina upande wowte lakin nashindwa kupima kasi maana naona hakuna freedom of speech kama zaman kwaio utofaut naouon na zaman saiv magufuli kawabana ule uhuru wakuongea ongea kama kikwete alivowaacha huru....ila kusem kuna kasi za ajabu labda kutumbua majipu na hasira na serikali imekua bingwa wa kuvunja sheria na taratibu
 
Ameandika haraka kiasi cha kwamba ameshindwa kuhariri andishi lake. Pole sana kama maono yako ni ya kitoto kiasi hicho.
 
Yaani umeandika utumbo mtupu na huna hoja,wapuuzi kabisa nyinyi,unawezaje kupima kasi ya siasa wakati wewe unakimbia na mwenzio amefungwa miguu,akili umeziweka wapi?unawezaje kusema makomeo anasimamia Sera za ccm wakati mpaka Leo hakuna ajira yoyote iliyotolewa na serikali hata waalimu wenyewe hamjawaajiri mpaka leo,hivi wewe ndiyo think tank wa ccm kweli? ndiyo maana hatupati maendeleo,
Unapozungumzia viwanda wakati Sera zinazotawala dunia ni za kikabaila huoni kama mnajitekenya wenyewe,serikali inazungumziaje viwanda wakati ilishasaini sheria na maelekezo kutoka mashirika ya fedha duniani ili kuruhusu mfumo wa soko huria? ndiyo maana alitakiwa kuhakiki hiyo degree moja,
sasa zile milioni 50 zilishagawanywa au unatokwa povu bure hapa,kama tayari mbona huku nanjilinji hazijafika na kama bado miezi 16 tayari huoni kama atatakiwa kutoa milioni 100 za miaka miwili au mlijua kuongoza nchi ni sawa na kumjengea nanihii kebys hotel?
OK,Sera za ccm sio kuwasomesha watanzania ndiyo maana hawapewi mikopo,lengo ni kuwa na malumpeni wengi ili kuwatawala vizuri,au siyo,
Hayo madawa ya kulevya mbona asilimia kubwa ni wanaccm na polisi mnaoshirikiana wakati wa kuiba kura au mnageukana
mrudisheni kwanza Ben saanane ili tuende sawa
 
Anajitekenya na kucheka mwenyewe! Chadema ingekuwa imepwaya mgekuwa mnahangaika nayo hivi? Unapotezaje muda wako kuandikia makala ndeefu hivi kitu kilichopwaya kisichokuwa na adhari tena kwako ccm?
Ccm mpya ndiyo kina Madabida, mzee wa ARVs fake? Huo upya wa ccm ni upi?
 
Watabisha kama kawaida yao
Mruhusu mikutano ya kisiasa muone kasi yetu.
Na wewe ndo walewale. Hivi mtu kama Lwakatare aliyeshindwa hata kujenga bsrabara jimboni kwake unaanzaje kumruhusu eti kuandamana, kwani aliomba kuwa mbunge wa jimbo ili alete maandamano? Hivi watanzania wanahitaji maandamano ama maji, afya na barabara?
 
Back
Top Bottom