Kura yangu itakwenda kwa mtu Shupavu, Jasiri asiyeogopa Mafisadi, Mwenye uwezo wa kukosoa lililo baya wakati wote bila kujali wala kuogopa macho ya rafiki zake wa karibu.
Hatima ya kura yangu haiamuliwi na CHAMA wala rangi za CHAMA, bali mtu mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika mfumo mzima wa uongozi. Inakwenda kwa mtu mwenye uchungu na matumizi mabovu ya rasilimali za watanzania yanayofanywa na serekali iliyopo madarakani. Si hivyo tu bali kura yangu itamlenga yule mwenye nia ya dhati ya kunyanyua ELIMU ya watanzania ili waweze kuendesha mali na utajiri wa nchi yao, kwa kuhakikisha ELIMU BORA inapatikana na inakuwa ni ya lazima kwa watu wote.
Nitampa kura yangu mtu mwenye Constructive aides, mwenye uwezo wa ku_reason na kutambua kuwa nchi nyingi zilikuwa masikini na kuamua kuwekeza kwa dhati katika nyanja mbalimbali mfano ELIMU, mwisho zikaweza kuwa mbali zaidi kiuchumi, kimaarifa, kisiasa na kiubora wa maisha. Nitampigia kura mtu anayeamini kuwa MAISHA BORA hayatafutwi majukwaani bali yanatafutwa kwa kuwekeza na kupanga mipango madhubuti tena ya muda mrefu.
Mtu anayechukia kwa dhati ufisadi na Mafisadi wenyewe ndio anayestahili kupewa kura yangu.
Asanteni sana