Kura yako ni sawa na risasi [itumie vizuri] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura yako ni sawa na risasi [itumie vizuri]

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BongoTz, Oct 26, 2010.

 1. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwenye hotuba aliyoitoa April 03, mwaka 1964 huko Cleveland, Ohio; Malcolm X, aliwahi kukaririwa akisema, "Kura ni sawa na risasi. Hufyatui risasi ovyoovyo mpaka kwanza uone shabaha, na kama shabaha hiyo iko mbali na wewe, jambo la busara kufanya, nikuirudisha risasi yako mfukoni."

  Well, zikiwa zimesalia takribani siku nne kwa watanzania wengi mijini na vijijini kuingia kwenye vituo vyao vya kupigia kura kumchagua mtu atakayeongoza Taifa letu kwa kipindi kingine cha miaka mitano, ni vema basi tukayatafakari maneno hayo ya busara toka kwa Malcolm X, na ikiwezekana, tuzitumie kura zetu vizuri siku ya Octoba 31.

  Tayari vyama mbalimbali vya siasa vimetangaza wagombea watakao viwakilisha vyama hivyo katika kinyang'anyiro cha Urais, Wabunge na Madiwani. Nia ya vyama vya upinzani/mageuzi kutaka kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni dalili nzuri kwamba demokrasia inazidi kukomaa na kuimarika nchini Tanzania.

  Swali tunalohitaji kuwauliza waliojitokeza kugombea Urais, Ubunge na Udiwani mwaka huu ni hili: Je, wamejipima kwa vigezo gani hata wakaona kuwa wanafaa kuwa Marais, Wabunge na Madiwani wa nchi yetu? Maana tunaambiwa kuwa wamo hata wale walioshindwa katika kuwajibika/tumika vizuri katika nyadhifa mbalimbali za kiserikali hata ikabidi waondolewe madarakani au walazimishwe kujiuzulu.

  Wamo pia wale ambao wana mipango ya makusudi kabisa ya kuligawa taifa letu la Tanzania kwa misingi ya udini na ukabila.

  Wamo pia hata wale ambao imethibitika kuwa wamechangia katika kulipotezea taifa mapato ya kodi kwa kutunga na kupitisha sheria karimu na mbovu za madini zilizowaneemesha wageni na kuliacha taifa letu katika hali ya umasikini wa kutupwa (technically, wabunge wote wa CCM wamo kwenye kundi hii).

  Wapiga kura nao wanahitaji kujihoji swali hili: kwanini watu hawa wanahitaji kuchaguliwa kuliongoza taifa hata baada ya mapungufu yote haya waliyoyaonyesha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita? Hivi wagombea hawa wanaojipaga kushiriki katika uchaguzi wa mwaka huu wanadhani watanzania hatuna upeo wa kina wa kufikiri, chambua na kufanya maamuzi mazuri ikiwezekana kuwaadhibu wale wagombea uchwara, mafisadi na wala rushwa kwa kupiga kura ya "HAPANA"?

  Ni imani yangu kuwa watanzania wote wenye umri wa kupiga kura mwaka huu hawatapoteza kura zao bure bali watahitaji maelezo ya kina na ya msingi toka kwa wagombea wote ili wapate fursa ya kuchambua na kuwachangua watu safi na bora wanaostahili kuliongoza taifa letu. Na sio maelezo ya kina peke yake, bali pia sera nzuri zinazoeleweka na kuonyesha ni wapi wagombea hao wamekusudia kulipeleka taifa letu katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.

  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!​
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Mungu mbariki slaa
   
 3. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa nitaitumia kwa yule ninae taka kumpa
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ballot not bullet
   
 5. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ballot it is...
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  And who's the target?
   
 7. R

  Renegade JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Zikiwa zimebaki siku nne kabla ya uchaguzi kura yangu ni kwa DR. Slaa, si hivyo tu, nimehakikisha kuwa hata mke wangu anampa Dr. Slaa, hiyo imekubalika tumeweka msimamo thabiti, lakini pia sikuishia hapo, nimetumia nafasi yangu katika familia kushawishi familia Yote ili wampigie Dr. Slaa, lakini cha ajabu ni kwamba nimekuta wote ni washabiki wa Dr. Slaa, hivyo katika jamaa ya watu kama 56,uzao wa baba yangu wote kura ni kwa Slaa. Wewe je ? Hujachelewa Amua sasa.
   
 8. T

  The King JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana. Endelea kuwashawishi wengine waliokuwa karibu nawe kama marafiki na hata majirani. 2010 ni mwaka wa mabadiliko makubwa nchini.
   
 9. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Well, it is not for me to tell you who or what the target should be. Use your own brain/make the right choice.
   
Loading...