Kura ya wazi itawaumbua CCM

Kura ya wazi itawaumbua CCM

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
CCM katika jitihada zake za kuiteka Katiba wametumia mbinu ya kuwanyamazisha wanachama wao walio kwenye bunge la Katiba wametumia mbinu ya kulazimisha kura ya wazi.

Walichofanya CCM ni kuangalia mambo kwa mtazamo mfupi sana na hawakuzingatia matokeo ya baadae muda si mrefu. Wamesahau kuwa kuna mambo mawili ambayo walitakiwa kuyatilia maanani hasa kwa upande wa Zanzibar.

1. Wamesahau kuwa siku zote ushindi wao unakuwa wa mizengwe kule Zanzibar au tuseme ni ushindi kiduchu.
Sasa uwazi una maana kuwa wapiga kura kwenye chaguzi na wananchi kwa jumla watawajuwa nani na nani ndio "wasaliti" wa maoni ya Wazanzibari hivyo basi wanabidi wajitayarishe na kushindwa na kunyooshewa vidole na wakazi wenzao. Hali inakuwa mbaya zaidi kwa wale wa makundi maalum wataishi vipi mitaani?

2. CCM imezoea kuwanunua wapinzani na kwa kukabiliana na hili umoja wa UKAWA utawaagiza wanachama wake wote nao wapige kura za wazi ili kuzuia usaliti kwa kununuliwa na CCM. Kwa upande wa Zanzibar wale watu 16 walioelezwa na rais hawatoweza kununuliwa.

Nategemea kuwa hii kura ya wazi itakuwa ni chaguo la vyama vya upinzani ili kuonyesha mtizamo wao wa serikali tatu na kuwafanya watakaopiga kura ya siri kuonekana wasaliti.
 
Mkuu una hoja nzuri lakini unahitaji kutulia na kuiandika vizuri zaidi.
 
Mkuu, Kanuni za bunge la Katiba hazilamishi mbunge yoyote kupiga kura ya wazi au siri.

Kilichofanyika ni wabunge kupewa uhuru wa kupiga kura ya wazi kama anapenda au ya siri vile vile kama anapenda, kwa maana nyingine, kila kundi lilipata kile lilichokuwa likitaka kuhusiana na aina ya upigaji wa kura. Hakuna mbunge au kundi la wabunge kwa sasa limelazimishwa nje ya matakwa yake katika aina ya upigaji wa kura

Andiko lako linaonyesha wewe ndiyo hujafahamu kilichokubaliwa au unafahamu lakini unajaribu kupotosha wana Jf.

Ni angalizo tu.
 
Acha uwongo,HAKUNA ANAELAZIMISHWA KUPIGA KULA YA WAZI,kanuni iliyopitishwa inamruhusu kila mjumbe kuamua ama ya wazi au ya siri na sio kama unavyosema eti wamelazimishwa.Na ndo maana hata mh Mnyika kapiga ya wazi.
 
Huielewi CCM wewe! Sasa kuna Mbunge wake anayetaka serikali tatu mfano, akajitokeza kwa uwazi na kusema 3? Ok huyo atapiga ya siri lakini tayari chama kitaelewa kapiga ya siri kwa vile anataka 3 kinyume na chama hivyo atashugulikiwa chini kwa chini. Na hilo la kushughulikiwa wabunge wa CCM wanalielewa sana.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
ha ha ha ha ha ha haaaaaah! Hapa vidumu vya tindikali vinawahusu wasaliti

Angalia vizuri hilo bango chini kulia! Kuna picha ya kisu na jambia. Hawa jamaa kwenye maslahi yao hawana blabla kama sisi huku bara. Na wakisema watakushughulikia ujue lazima wafanye hivyo.
Ngoja tuone maana walao wameshatoa onyo.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mkuu, Kanuni za bunge la Katiba hazilamishi mbunge yoyote kupiga kura ya wazi au siri.

Kilichofanyika ni wabunge kupewa uhuru wa kupiga kura ya wazi kama anapenda au ya siri vile vile kama anapenda, kwa maana nyingine, kila kundi lilipata kile lilichokuwa likitaka kuhusiana na aina ya upigaji wa kura. Hakuna mbunge au kundi la wabunge kwa sasa limelazimishwa nje ya matakwa yake katika aina ya upigaji wa kura

Andiko lako linaonyesha wewe ndiyo hujafahamu kilichokubaliwa au unafahamu lakini unajaribu kupotosha wana Jf.

Ni angalizo tu.

Mfumo wowote wa KIdemokrasia unataka mtu apige kura ya siri,hii ni kutokana na kutokuwa infuenced na mtu au kitu chochote wakati wa kupiga kura.Kilichofanyika kwa CCM ni kuwanyima uhuru wana CCM wa kuvote against, kwani ilikua inaangalia ni kina nani watakao vote against.Ilikua rahisi kwa CCM wale wanaovote kwa siri ni dhahiri hawako upande wao, na wale watakaovote wazi wanajulikana.
Huu ni uhuni.Kwani viongozi wenyewe wa bunge walichaguliwa kwa kura ya siri.
 
Msingi na Kigezo cha demokrasia ni kufanya jambo kwa matakwa yako ambayo wakati mwingine unaweza kuyaweka kisheria ili kuwepo na kumbukumbu katika utendaji wake.

Bunge la Katiba kwa kupitia kanuni zake limeamua kuwaacha wabunge kupiga kura kwa matakwa yao. Anayetaka kura ya siri, atapiga kura ya siri. Anayetaka kura ya wazi atapiga kura ya wazi.

Kabla ya kupata maafikio hayo, wabunge waliulizwa kama wanaafikiana na mapendekezo halafu hapo hapo walipewa option ya wazi au siri kupiga kura zao. Kilichostaabisha ni kuwa, walioenda kupiga kura za siri walikuwa ni 72. Katika hizo kura za siri, walioafikiana na mapendekezo walikuwa ni 26 sawa na 36% ya walipiga kura ya siri na 46 hawakuafiki mapendezo.

Kwa fikra zako, hawa 26% walipiga kura ya siri lakini wakaafiki mapendekezo ya kura ya mseto walitoka chama gani.
 
Acha uwongo,HAKUNA ANAELAZIMISHWA KUPIGA KULA YA WAZI,kanuni iliyopitishwa inamruhusu kila mjumbe kuamua ama ya wazi au ya siri na sio kama unavyosema eti wamelazimishwa.Na ndo maana hata mh Mnyika kapiga ya wazi.
Bora ya mimi kuwa muongo lakini wewe kuwa mnafiki kunakusaidia nini, zile siku 40 zilikuwa za nini?
 
Mkuu, Kanuni za bunge la Katiba hazilamishi mbunge yoyote kupiga kura ya wazi au siri.

Kilichofanyika ni wabunge kupewa uhuru wa kupiga kura ya wazi kama anapenda au ya siri vile vile kama anapenda, kwa maana nyingine, kila kundi lilipata kile lilichokuwa likitaka kuhusiana na aina ya upigaji wa kura. Hakuna mbunge au kundi la wabunge kwa sasa limelazimishwa nje ya matakwa yake katika aina ya upigaji wa kura

Andiko lako linaonyesha wewe ndiyo hujafahamu kilichokubaliwa au unafahamu lakini unajaribu kupotosha wana Jf.

Ni angalizo tu.

Naona unakuja na hoja dhaifu sana tena sana unless unakusudia kuuendeleza uCCM!
Hivyo unafikiri sote tuna uwezo sawa wa kufikiri. Ni sawa uwezo wako wa kufikiri umekufanya uamini unavyoamini na mimi nina mtazamo tofauti wala usinione kuwa sina uelewa.
Hata hivyo ninachokieleza mimi ni kuwa huo uchaguzi wa CCM katika mfumo wa kupiga kura, kama walikusudia uwanufaishe basi wajitayarishe na upande wa pili wa shillingi yaani taathira mbaya kwa uamuzi wao.

Jee na wewe hujaelewa bado?
 
Mkuu, Kanuni za bunge la Katiba hazilamishi mbunge yoyote kupiga kura ya wazi au siri.

Kilichofanyika ni wabunge kupewa uhuru wa kupiga kura ya wazi kama anapenda au ya siri vile vile kama anapenda, kwa maana nyingine, kila kundi lilipata kile lilichokuwa likitaka kuhusiana na aina ya upigaji wa kura. Hakuna mbunge au kundi la wabunge kwa sasa limelazimishwa nje ya matakwa yake katika aina ya upigaji wa kura

Andiko lako linaonyesha wewe ndiyo hujafahamu kilichokubaliwa au unafahamu lakini unajaribu kupotosha wana Jf.

Ni angalizo tu.

Sawa kabisa Mkuu hivyo ndivyo inavyopasa iwe
 
Back
Top Bottom