Wana bodi kutokana na mambo mengi ambayo yamkini kila mwanaharakati amekuwa akiyaona yakifanywa na ndugu huyu mengi yakiwa na mtizamo hasi na chama napendekeza ipigwe kura ya maoni iwapo huyu bwana (simuiti mh. mbunge wanabodi mtanisamehe kwa hilo) aendelee kuwa mwanachama wa chama kikubwa kama hiki cha ukombozi au avuliwe uanachama.Nimeshawishika kuleta wazo hili kwenu nikiwa na imani kabisa kuwa wapo wengi kama si wote ambao wanachukizwa na vituko anavyovifanya huyu jamaa yakiwemo matamshi yake bungeni rejeeni hoja ya posho ya wabunge na nyinginezo nyingi. nawasilisha