Kura ya kutokuwa na imani na mbunge.

FortJeasus

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
603
397
Baada ya mjadala mkali wa takribani wiki mbili sasa,ndani na nje ya bunge,kufuatia ripoti ya CAG,na ulioibua shinikizo dhidi ya mawaziri kadhaa kujiuzulu nafasi zao kutokana na makosa ya uwajibikaji,na ambao hata hivyo hawakufanya hivyo na shinikizo hilo kuhamishiwa kwa Mizengo Pinda kwa kuanzishwa na hatimaye kukamilika mchakato wa kupata asilimia 20% ya majina na sahihi za wabunge,na hatimaye leo kupatikana taarifa za Kamati Kuu kingilia kati sakata hilo,nimepata wazo kwa nini kusiwepo uwezekano wa kuwaondoa wabunge dhaifu kiutendaji kutoka nafasi zao kabla hata hawajamaliza kipindi cha miaka mitano cha uongozi wao.
Msingi wa hoja hii ni Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,inayoweka wazi kabisa kuwa msingi,mamlaka na uhalali wa serikali kutawala utatoka kwa wananchi wa Tanzania.Kwa kuwa wawakilishi wetu ,kwa niaba yetu,wana nguvu ya kuwaondoa Waziri Mkuu na hata Rais kwa kuwapigia kura za kutokuwa na imani nao,sasa, ni wakati muafaka kwa wananchi kuweza kuitumia nguvu yao hiyo,wao wenyewe moja kwa moja, yenye msingi,mamlaka,na uhalali wa Kikatiba kuwafanya wawakilishi wao wawajibike kwao kwa kuwapa wanananchi uwezo,uhalali na mamlaka kuwaondoa wawakilishi wao kwa kupigia kura ya kutokuwa na imani na mbunge ikiwa hafanyi kazi ipasavyo.Mathalani,wananchi wa Jimbo la IGUNGA wangeweza kabisa kumweleza mbunge wao Kigwangala kuwa ahh!bwana mbunge, umeshindwa kuisimamia serikali bungeni kwa kutotia saini karatasi ya Ndugu Zito,kinyume na Makubaliano yetu kuwa ikiwa ungeshinda ubunge ungeiwajibisha serikali,tunaomba ukae pembeni!
Kenya,kwa mfano,katiba imewapa wananchi uwezo huo kwa kuwapa wananchi haki na nguvu ya petition to parliament.Wakati wa uchaguzi mkuu,wagombea wote wa vyama vya siasa katika kila jimmbo la Uchaguzi,huingia Makubaliano ya kimaandishi-yanayotofautiana kutoka Jimbo moja hadi jingine kulingana na vipaumbele-yenye nguvu ya kisheria na wananchi wao ,na wananchi huweka wazi matarajio yao na Wabunge huweka dhamira ya kufanyia kazi Makubaliano hayo kwa kuweka saini mkataba huo.Mgombea anayeshinda uchaguzi, na kwa sababu mbali mbali kushindwa kutenda kulingana na makubaliano, wananchi wa Jimbo husika wanaweza kuanzisha mchakato wa kukusanya majina na saini za wananchi ,na zinapofikia idadi fulani, kura ya kutokuwa na imani Mbunge hupigwa mara moja.
Sasa,kwa nini nasi tusiwe na utaratibu huo?
Hili haliwezi kuwa miongono mwa masuala ya msingi katika katiba mpya?
Tujadili.
 
Naunga mkono.. Na katiba la nchi yetu halitoi mwanya wa notisi Kwa waheshimiwa hawa. Ila kuna mpito wa soundmind ambao ni mchakato wa kutembeza maelfu ya Saini Na kupeleka kwenye vyombo vya habari Kwa shinikizo la kuachia kiti.. I mean it Na lazima tuianze.. Nchi yetu, wananchi ndo sisi wenyewe nani atusumbue tumwachie?
 
Back
Top Bottom