Kura ya kupitisha bajeti yapigwa bila kambi ya upinzani kuwepo bungeni, yapita kwa kishindo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Wakuu,

Leo jioni wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wameanza kupiga kura ya ama kuipitisha ama kuikwamisha bajeti ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bajeti ni kitu muhimu hasa kwa sababu ina mchango mkubwa wa kuamua mustakabali wa mwaka ujao wa fedha pamoja na siku nyingine zijazo.

Kuna mambo mawili ya kusikitisha nimeyaona, kwanza kura zinapigwa bila kuwepo sehemu ya wabunge(wabunge wote wa upinzani) lakini pili ni kwa wabunge wote waliobaki wote kuwa na akili moja hata wale ambao mwanzo walionekana kutoridhia, yaani nasikia neno moja tu tangu kura zianze. Kuna haja wabunge wa upinzani na wa chama tawala watafakari tulichowatuma bungeni.

Zoezi la upigaji kura limekamilika na bajeti hiyo imepita kwa kishindo

Wakuu,

Leo jioni wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wameanza kupiga kura ya ama kuipitisha ama kuikwamisha bajeti ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bajeti ni kitu muhimu hasa kwa sababu ina mchango mkubwa wa kuamua mustakabali wa mwaka ujao wa fedha pamoja na siku nyingine zijazo.

Kuna mambo mawili ya kusikitisha nimeyaona, kwanza kura zinapigwa bila kuwepo sehemu ya wabunge(wabunge wote wa upinzani) lakini pili ni kwa wabunge wote waliobaki wote kuwa na akili moja hata wale ambao mwanzo walionekana kutoridhia, yaani nasikia neno moja tu tangu kura zianze. Kuna haja wabunge wa upinzani na wa chama watafakari tulichowatuma bungeni.

Ni sawa tu waache ccm watii kiu yao, kuna siku watajutia matendo yao!
 
Back
Top Bottom