Kura ya elektronik ndio inafaa

Kura ya elektronik ndio inafaa

Paul Makonda

Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
97
Reaction score
185
Tukielekea Kwenye Mjadala wa Leo Jioni Hii:

Tumekaribia kufikia makubaliano ya jinsi ya kupiga kura ya maamuzi. Makubaliano yoyote yawe kwa misingi ya kulinda maslahi ya taifa na heshima ya bunge hili. Pamoja na kuwa watanzania wengi hawatuelewi katika mijadala yetu kama kweli tuna nia thabiti ya kutengeneza katiba ya Jamhuri.

ubishani wa aina gani ya kura tutaitumia, unatakiwa ufike mwisho. Ama kura za wazi ama za siri ni mambo yanaweza kwisha. Kuna kura ya Kielektronic ambalo nalo laweza kuwa wazi ama Siri.
Kwa mujibu wa mabadiliko ya kanuni kupitia kamati ya Kanuni na Maridhiano. Imetoa maadhimio ya ama SIRI ama WAZI.

Mjadala huu unaenda mbali kwenye kulazimishana sasa wale wa WAZI wanawavuta wa Siri na wale wa SIRI halikadhalika wanawavuta wa Wazi.

Sasa, kwa nini wote tusiachane na hizo kura za WAZI ama SIRI za Makaratasi na twende kwenye DIJITALI yaani Tuingie kwenye ELECTRONIC VOTING.

Mivutano ya Wazi au Siri ni ya kimakundi. Haina Maslahi na Taifa na daiyo maana makundi haya yameanza kutafuta ushawishi wa kundi kuungwa mkono na wajumbe wengi kuliko jingine. Na kama tukiacha hali hii iendelee, tutajikuta tunatakiwa tupumzike siku mbili au tatu kwa ajili ya watu kupiga kampeni za kuhamishana huku na kule. Na kupumzika nakokusema si lazima kuwe rasmi maana kuna watu humu wanaweza kuja na Vurugu zisizo na maana na kulazimisha Mwenyekiti ama Makamu Mwnyekiti kuahirisha Bunge hili Maalum.

Tuhame kwa pamoja, ELEKTRONIK ndo Mpango wa kutuondoa katika Mgogoro huo. Mfano mzuri wa Kura za Elektronik ni Mifumo ya Kura za Maoni Marekani, Mataifa ya Ulaya na hivi Juzi Kenya. Tofauti ndogo ya sisi hapa na huko ni kwamba huko wanatumia njia ya Mtandao kupiga kura kwa Internet na kisha unapata Majibu mara tu baada ya Uchaguzi. Uholansi wanatumia Elecronik kwa uchaguzi Mkuu.

Kura ya Kielektronik.
Tutapiga kura kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa tunavyotumia kwa mawasiliano humu bungeni na kura zote zitahesabiwa na machine (Mtambo maalum) na tutapata majibu sahihi ya kweli yasiyo na shaka ya uhalali wake.

Wapo wanaojenga hofu eti Mfumo huu ni wa Wizi. Hapa tuwaeleze kuwa Electronic ni ya Kuaminiwa ndiyo maana kuna watu wanasomea kwa miaka mingi. Na kama Kuna Alegations kuwa huo ni Mfumo wa Wizi, basi na ithibitishwe kuwa waliosomea wamesomea Wizi.

Tutafanya kazi hiyo kwa muda mfupi sana na kwa muda mfupi huo tutapata majibu. Sasa hapo ukitaka UWAZI au USIRI hiari yako maana kwa wale wa WAZI watapata PRINTOUT ya Kura zote na Kila mtu kwa Jina lake, na Wale wa SIRI wataachana na Kupata hiyo PRINTOUT.

Elektronic itaendelea kutuweka wamoja wenye kupingana kwa Hoja bila Kupigana litakapofika suala la Kuamua Kwa Kura. Pamoja na Changamoto zake Mfano a ni upatikanaji wa nishati ya Umeme kwa muda wote, na
Inahitaji kujiridhisha na kufanya majaribio, lakini ukilinganisha na Changamoto, Faida ni nyingi na zenye mantiki kuliko Changamoto.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda,
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba
 
Ujinga mtupu
Hao wabunge wanaotaka kura ya wazi wao walichaguliwa kwa kura ya wazi??
Ccm mna matatizo sana hata wewe mleta mada acha kudharau Wananchi, yaani hatujui ni nini mnashindana??
Iko siku mtajua tunawafahamu kuliko mnavyo fikiria. Mko kwa ajili ya matumbo yenu na sio kwa maslaji ya Watanzania. Mnawalisha wajumbe hongo ili wakubaliane na mawazo ya ccm, hii ni aibu na matusi kwa wananchi. Hii sala yako hapa pia ni ya kinafiki. Sikutegemea kiongozi mwenye dhamana ya naibu katibu mkuu wa chama pia waziri anaongea matusi na bungeni , bunge linaloangaliwa na mamilioni ya watu ndani na nje ya nchi. Hiyo ndiyo ccm ya Karume na Nyerere kweli???
 
Hapana tumieni paper tu za kawaida kura zihesabiwe manualy


Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Paul Makonda,kama mnakaribia kufikia makubaliano haraka ya nini kuja hapa na kuweka kama makubaliano tayari? Kuwa mpole na usubiri maamuzi kamili huko uliko
 
Last edited by a moderator:
Mpate print outs ili mkatuadabishe baadae hiyo nayo hatutaki, tunataka siri ambayo hakuna mtu atajua kwa namna yoyote mimi au yule alifanya maamuzi gani
 
Kwanini msikubaliane kuupigia mtafaruku huu kura ya siri? Kama watakaosema wazi ni wengi basi iwe ni wazi na kama watakaosema siri ni wengi basi iwe siri.
 
Hoja hapa ni ama kura ya siri au wazi na sio 'tool' gani itumike kufanikisha upigaji kura.

Sijui mleta hoja anataka kusema nini kwa sababu 'elecronic voting system' bado inaweza kuwa set ili ijulikane nani kapiga kura vipi.
 
Kila kifaa cha umeme kina address sasa usiri utatoka wapi?
Kwa mfano labda Paul Makonda anakaa kiti namba 127 na address ya kigaa chake ni mcx23703hk sasa kama watu wanataka wajue ulichagua nini wanaahindwa nini, ukweli ni kwamba kuta ya kielekroniki haina usiri ni sawa na ya wazi.
 
Ningewaona CCM mna nia ya dhati ya KATIBA mpya kwa vizazi vijavyo kama mngewapa wajumbe uhuru wa kuamua.Kuna watazania ambao ni waumini wa Serikali mbili lakini tunahitaji wajumbe waargue kwa hoja zenye mshiko na siyo kuwaburuza.Wapeni uhuru na the best kutumia ni KURA YA SIRI.

Sioni kwa nini CCM muogope KURA ya siri ilhali mko wengi.Wekeni Confidence kwamba uamuzi wowote utakaopitishwa mtashinda.

Pili msiweke mchakato huu kuwa wakiCCM ,muelekezeni Mwenyekiti wenu kuwa kuwe na haki sawa kwenye representation kwenye KAMATI YA UONGOZI.Mkifanya hayo mtakuwa mmeuweka mchakato huu kuwa bora na wenye nguvu.Acheni kutumia hoja ya nguvu tumieni nguvu ya hoja.

Paul Makonda wewe ni kijana waheshimu vijana wenzako wapiganie kwa lengo la kuweka uhuru wa kujieleza,waonyeshe vijana wenzako nini kinachotakiwa kufanywa na CCM bila kuweka ushabiki wa vyama.Waeleze wale wazee ambao toka nipo darasa la pili mwaka 1975 kuna watu ni wabunge hadi leo,jiulize kama hawakuweza kuiletea maendeleo miaka yote hiyo je leo watakuwa na uwezo wakutuletea katiba tuitakayo?Waangalie vijana wamiaka 20 leo KATIBA isiyo na manufaa kwao ya nini?Waoneeni huruma hawa,msiwaachie WAZEE wa miaka 65-70 wawaaamulie vizazi vijavyo,mtajichora kwa vijana wa miaka ijayo.

Kama itashindikana basi vunjeni BUNGE ili kile kidogo kilichobaki kirudishwe kwenda kuboresha daftari la wapiga kura,afya au elimu.Tuoneni huruma watanzania wanyonge na maskini.
 
we jamaa hamnazo kabisa, yaani unakuja na suruhisho la kitoto hivi kisa ni nini? kweri ccm ni wapuuzi kuliko wapuzi wote duniani, yani mmeshindwa kujenga hoja kwa nini ya siri hamtaki na kwa nini mnataka ya wazi mnakuja kupiga porojo kama mazuzu mitandaoni, malipo yenu ni hapa hapa chini ya jua wehu nyie
 
mchumia tumbo wewe, unatumika kwa maslahi yako binafsi!........evod manda ameshakujibu kuwa kamati imeona haifai kwani ni rahisi kuchakachuliwa!

Ulisema kuwa vifaa hivyo vya kielekronik vya kupigia kura vimeshanunuliwa tayari (kwa kodi za wananchi)......sasa hao walionunua hiyo mitambo, kawaambie warudishe fedha zetu.....na nani waliwaagiza wakainunue!
 
Wapo wanaojenga hofu eti Mfumo huu ni wa Wizi. Hapa tuwaeleze kuwa Electronic ni ya Kuaminiwa ndiyo maana kuna watu wanasomea kwa miaka mingi. Na kama Kuna Alegations kuwa huo ni Mfumo wa Wizi, basi na ithibitishwe kuwa waliosomea wamesomea Wizi.

[/B]

Nakubaliana na usemi kuwa ukiwa ccm akili inadumaa. Hivi hujasikia watu wamekamatwa kwa kuiba kwenye atm, au hiyo síyo elektroniki?

hujasoma kuhusu mkenya aliyekamatwa kwa kuunganisha simu za kimataifa na kuiibia tcra? hiyo siyo elektroniki?

Kwa mifano hiyo miwili ndiyo, waliosomea elektroniki wamesomea wizi. hivyo pendekezo lako la kura ya elektroniki halíkubaliki.

Na mwisho uachane na imani yako ya kudhani watz wote ni wajinga.
 
Hawa si ndio watoto ambao baba zao ndio walikuwa vigogo wa CCM,waache watambe,kosa ni la baba zetu kuwaamini baba zao kuwa ni wenzetu,na sasa wanatutia vidole midomoni,wao ndio wanajua kila kitu kwa hiyo sisi tukiwa kama madodoki tuwafuate tu wao,wao ndio wenye hekima sisi wengine ndio wajinga
 
Ile ndege ya malaysia iliyobeba watu 239..wasio na hatia wakapotea.Bora ingewabeba wajumbe(wabunge) wa katiba ikapotea nao kuliko vitu wanavyofanya Bungeni.
 
Back
Top Bottom