Noncommited
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,125
- 369
Wasalaamu wana Jamvi!
Leno ningependa niwasilishe mada moja inayojadili Umuhimu wa KURA moja tu ya Urais katika chaguzi za Tanzania.
Kwa Tanzania KURA muhimu na ya ushindi ni ya Urais tu nyingine zote zina umuhimu madogo sana kama Mkuu wa Nchi akijali Demokrasia na kama hajali Demokrasia basi KURA za Ubunge, Udiwani na Uenyekiti wa mtaa au kitongoji hauna umuhimu.
Nitatoa mifano Michache:
Mbunge yeyote awe wa CCM au Upinzani anadhibitiwa na kuwa chini ya Mkuu wa Wilaya husika au Mkuu wa Mkoa. Mbaya zaidi akiwa wa chama cha Upinzani atadhibitiwa vilivyo hana chake zaidi ya kuzungumza bungeni na hata akitoa pesa yake mfukoni kuhudumia wananchi anaweza kuzuiliwa kama alivyofanyiwa Mbunge .Wilfred Lwakatale kule Bukoba wafanyakazi wa Hospitali waliikataa misaada yake ya vifaa tiba na pia uchangishaji wa michango ya maafa ya tetemeko la Bukoba 2016. Pia kuna mbunge wa Songea mjini na baraza lake la madiwani maamuzi yao ya kurudisha stand kuu katikati ya mji yalizuiliwa na Mkuu wa mkoa. Mifano iko mingi sana wadau pia mtaisaidi kuiorodhesha
UPANDE WA DIWANI
Madiwani wanadhibitiwa hasa na watendaji wa kata wana ziwakilisha kwa kila maamuzi wanayoyafanya hasa wale wa Upinzani.
MWENYEKITI WA MTAA/KITONGOJI
Hawa wanadhibitiwa na watendaji wa Mtaa na wa kata. Huwa hawafurukuti kwa kwa watendaji hao na akiwa Duiwani wa upinzani ndio kabisa.
KURA muhimu na yenye nguvu ni ya Urais tu. Hii inatokana na jinsi katiba inavyombeba Rais kuliko kiongozi mwingine yeyote tofauti na nchi zinazotumia mfumo wa majimbo.
Nawasilisha