Kupotea na kutekwa kwa watu, Watanzania tunatumiaje siku ya kimataifa ya kupinga "kupotezwa"?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,805
1,874
NI wazi kwamba watanzania wengi sasa wanajua tu kutumia siku kama ya wanawake yaani "International Women's Day", tena napo haijapita miaka kumi tangu kelele kuhusu siku hii kufanyka kama shereha na maandamano ya wanaake.

Kwa hilo tumepiga hatua, kila iifika March 08 ni lazima shamrashamra na viongozi wa serikali wakimeo kuihamasisha siku hii.

Kuna wakati kuna mbunge mmoja alipendekeza iwe ni siku ya mapumziko akajibiwa kwamba sipo "Internationa Days" nyingi na huwezi kuziweka zote ziwe siku za mapumziko.

Sasa wiki y apili sasa tunapiga kelele kuhusu utekaji, tena utekaji wenyewe wa watu wachache tu hata kama ni kweli wako 11 katika ile list.

NImepitia historia katika magazeti yetu kwa miaka kadhaa, hakuna hata siku moja wala hakuna mtu hata mmoja hapa Tanzania aliyewahikuhamasisha siku iitwayo International Day for the Disappeared. Hii kwa miaka yote imekuwa ikifanyika August 30 ya kila mwaka.

Narudia, sijawahi kuona hata siku moja, si mwandishi wa habari, si polisi, si serikali, si mbunge, si jaji au hakimu, si wananchi, si Jamii Forum au mtandao wowote, yaani hakuna hata mmoja wetu anayetaka ijulikane kwamba hiyo siku ipo.

Tuko kimya tunaendelea na kelele ambazo baada ya mwezi tu zimekufa kama ngoma yoyote ya msimu.

Wakati hii ndiyo siku ya kuandamana hadi sehemu kama Kinondoni,wananachi wanasoma orodha ya watu waliopotea na hawajapatikana.

Kama ni D'Salaam anakuja mkuu wa mkoa wa D'Salaam anajisifu jinsi mkoa wake usivyokuwa na watu waliopotea na hata waliopotea wamepatikana anatoa nasaha zake anavyochukia utekaji na kupotea kwa watu.

Kisha inakuja serikali inasema nayo inakuja na rodha yake ya watu waliopotea na ikawapata na hapo wakati huohuo serikali inajibu hoja za wananchi kuhusu listo ya wananchi kuhusu waliopotea.

Sasa, haya hayafanyiki.

Ikifanyika kila mwaka yaani August 30, kama inavyotakiwa, huku taasisi za kimataifa kama UN, haki za binadamu zinaalikwa kwenye maadhimisho hayo, basi serikali itapenda kuonyesha ushujaa kwenye jumuiya ya kimataifa jinsi inavyokerwa na utekaji na inavyolinda watu wasipotee.

Kama serikali inazembea basi siku hii imepangwa kuziumbua serkali ambazo wananchi wake wanapotea tu na wananchi hawajui eti na serikali nayo inalalamika tu.

Hivyo, mwaka huu itakapofika August 30, 2017 ninatarajia hizi kelele za kupotea Ben Saa Nane, na hata wengine wengi zitatikisa siku hiyo.
 
Inategemea na Maslahi ya siku yenyewe kwa hao unawaita wahamasishaji.

Kumbuka mwaka 1992 December 18 UN ilipitisha azimio kuwa ni kosa kwa Serikali kuwateka watu na kuwapoteza kabisa baada ya nchi zaidi 30 kuripoti visa vya kupotea watu bila taarifa.

30 August 2007 nchi ni Philippines watu zaidi 46,000 walitekwa na kupotea kwa nguvu ya mikono ya vikosi vya usalama kiasi cha mwaka uliofuata waliadhimisha mwaka mmoja watu kupotea na ndiyo ikawa siku ya kupotea watu duniani.

Je vyombo vya habari vitauza hizo habari,serikali itaruhusi hizo events ktk public,wafadhili watatoa pesa siku ya uhamisishaji n.k

Huyo siku IPO kwa wanaharakati lakini bado sana kujulikana kwasababu haina positive results ..waliopotea hawarudi,watu wengine walishakuwa majivu,mifupa,matahira n.k wanarudi vipi???
 
Mkuu nakubaliana na wewe na haya ndiyo majibu ninayotarajia kutoka JF.

Cha msingi walau kuwe na kelele tu inatosha maana kama huna sila za kushindana na watekaji basi hata kelele zinatosha na ndiyo maana maaskofu hawahan risasi hata moja lakini kelele yao serikali zote hunywea.

Tusiipuuze siku hii kwa sababu eti haina matokeo positive.
 
Basi issue hapa ni kukusanya data za watu waliopotea ili kuwa na takwimu sahihi za kitaifa.kwa specified period
 
Back
Top Bottom