Kuporomoka kwa elimu Tanzania: Jinsi waandishi wa vitabu wanavyowadumaza wanafunzi kifikra

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
304
236
TANZANIA ina upungufu mkubwa vitabu vya elimu kwa ajili ya kufundishia (kiada) na kujifunzia (ziada) jambo ambalo limechangia ongezeko la waandishi wengi.

Kuibuka kwa wimbi la waandishi wengi Watanzania kumefanya kuwepo na baadhi ya vitabu ambavyo vina muundo unaomfanya mwanafunzi kukariri badala ya kuelewa, huku vingine vikiwa na vitu vichache kiasi kwamba inakuwa haina tofauti na notisi za mwalimu.

FikraPevu inafahamu kwamba, vitabu ni sehemu ya kuongeza uelewa na ujuzi wa vitu kwa mwanafunzi, lakini kwa mwalimu pia ni sehemu ya kufanyia maandalio ya mamsomo kwa kuchukua baadhi ya vitu ambavyo anaweza kwenda kufundishia darasani.

Kwa maana nyingine, vitabu hivyo vinatarajiwa kuwa na vitu vingi vya ziada kwa mwanafunzi na hata mwalimu, ambaye mambo anayofundisha darasani yanatakiwa kuwa kama mwongozo ili mwanafunzi anaporejea kwenye kitabu ajifunze zaidi.

Lakini vitabu vingi vinapoandikwa katika mtindo wa ufupisho (summary) kwa kutoa maana ya maneno tu au baadhi ya vitu hii huwafanya wanafunzi kukariri na walio wengi huishia kusoma notisi ambazo wamepewa na walimu wa shule au katika masomo ya ziada (tuition) kwa kuona hakuna tofauti kati ya vitabu na kile ambacho wamepata kutoka kwa walimu hao.

Kufahamu zaidi, tembelea => Waandishi wa vitabu vya ziada na kiada wanawadumaza wanafunzi kifikra
 
Mimi daima huwa nasema, tumeamua kuishi maisha yasiyo yetu hivyo lazima tutakuwa nyuma!
Huwezi kulinganisha uandishi wa vitabu wa kiAfrika na wa mamtoni maana kwao formal education imeanza kitambo mno.
 
Hilo uko sahihi sana, kuna vitabu vimechapwa na Oxford press, vyenye waandishi mbalimbali na ni vitabu tofauti ni vitabu vya hivyo hovyo sana.

Havifai kutumika kufundishia wala kujifunzia lakini ndivyo vilivyojaa mashuleni.
Hakuna kitabu kilichochapwa na Oxford press hakina makosa,vyote vina makosa mengi sana tatizo waandishi WA vitabu hivyo ni WA hovyohovyo kabisa. Havifai kutumika
 
Elimu kwetu sio kipaumbele kiviiiile atleast sio kwa vitendo. Blah blah nyingi, washika dau wanapeleka watoto wao nje ya nchi huku bora liende tu. Nashukuru nilisoma shule nzuri nikawa na access na vitabu mbalimbali hata uelewa wangu wa vitu nilivyosoma enzi hizo ni wa Kumshukuru Mungu.
 
Hilo uko sahihi sana, kuna vitabu vimechapwa na Oxford press, vyenye waandishi mbalimbali na ni vitabu tofauti ni vitabu vya hivyo hovyo sana.

Havifai kutumika kufundishia wala kujifunzia lakini ndivyo vilivyojaa mashuleni.
Hakuna kitabu kilichochapwa na Oxford press hakina makosa,vyote vina makosa mengi sana tatizo waandishi WA vitabu hivyo ni WA hovyohovyo kabisa. Havifai kutumika
oxford press ya India nadhani hata Oxford University wenyewe hawajui haya matoleo. Uchina na uhindi dugu moja.
 
Back
Top Bottom