Kupitia video hii Polisi vs CCM, naomba nitoe MAONI yangu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,513
Kupitia video hii, naomba nitoe MAONI yangu kwamjibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kifungu cha 18 (1) na (2). Nasema kwamba ni wakati sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama hususani jeshi la polisi kufanyiwa mabadiliko makubwa na kuliondoka katika makucha ya siasa za vyama.

RPC wa Geita ameonyesha weledi na ukomavu mkuu kulitetea jeshi letu na siasa chafu za kivyama. Bila kujali kuna ugomvi binafsi katika ya RPC na hao makada wa ccm au laaa, lakini kama ningekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, kwa hatua hii ya RPC wa Geita ningemtunuku nishani ya ushujaa, Chama cha mapinduzi kimelitumia jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na kuvinajisi kwa kila aina ya siasa chafu.

Ni wakati wa jeshi la Polisi kuwa huru, uhuru wao hautakuja tu kwakujipendekeza kwa wanasiasa bali kuliondoa jeshi katika muondo wa siasa za kivyama.

Maendeleo ya nchi yamefeli na yataendelea kufeli kwasababu ya muundo wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ni wakuhami chama tawala zaidi badala ya kuhami taifa na uchumi.
Mfumo mbovu vya vyombo vya dola ndio unaoleta ghasia za umma katika jamii ya kisiasa, mfumo mbovu wa vyombo vya dola ndio uliotoa mwanya Rais kwa matakwa yake kuzuia shughuli za kisiasa kinyume na katika na sheria za nchi.

Rais wangu Magufuli, kinachoongoza nchi ya uchumi na viwanda vihubiriwavyo ni mfumo bora na thabiti wa ulinzi na usalama, hapa pakiwa na mfumo imara unaohami uchumi badala ya kuhami ccm ni kazi BURE KABISA. Chochote unachokifanya sasa bila kugusa mifumo hii ya ulinzi n usalama ni kazi bure, nasema hivyo kwakuwa mifumo ya kuzaa taifa la uchumi na maendeleo ni ileile aliyoiasisi Mzee wetu Julius Nyerere, ni ileile ya kijamaa iliyofeli 1992 pale Zanzibar, ni ileile ya ujima.

Tanzania haihitaji mtu mkali au mpole, haihitaji mtu mchapakazi au mvivu, bali inahitaji mifumo mipya ya Kiulinzi na kiusalama yenye anuwai za kiuchumi nasi hii ya kudumisha madaraka na utawala unaoendelea kudumaza taifa na kutia woga umma kwa mwamvuli wa chama dola.

Waziri wa Mambo ya ndani kaka yangu Mwigulu Nchemba, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Fedha na Uchumi, ni wakati sasa ya kukaa pamoja na kung'amua kuwa dunia ipo katika sayari nyingine kiulinzi, kiuchumi na kikatiba na kisheria. Wakati wa kudumisha utawala wa vyama vya siasa umepitwa na wakati.

Rais wangu mpendwa Magufuli, ruhusu mabadiliko ya vyombo hivi ili uweze kufanikisha nchi ya viwanda, ruhusu mabadiliko ya katiba mpya, ruhusu mabadiliko ya sheria nk, Taifa litakuandika kwa wino wa dhahabu kwa mabadiliko hayo.

Na Yericko Nyerere
 
Attachments

Mengine tunahitaji Maombi tu kwani maombi ni sera ya serikali yangu.
 
Embu tusubiri chief (mkuu wa wachawi) kanda ya ziwa atamfanyaje huyo rpc of course ni RPC uchwara..
Hapa namuona mkuu wa mkoa wa m.. Anavizia kakitu fulani Muda huu..
 
Itakuchuku mda mrefu kuelewa siasa!vipi kile kitabu chako ulichotafsiri bila kumtambua mwandishi kinaendeleaje?
 
Jk, aliwai kuwaambia. maccm kuwa wasitegemee mapolisi kufanya siasa kwani wataaibika sana huko mbeleni.
 
nilisikia ga ulikula pesa ya kanisa vipi ulikwisha lipa au unaendelea kupata laana ya kanisa
 
TUNDULISU HAYUPO LAKINI BADO WANAUMBUANA

JE WATUWASOJULIKANA MTAUA WANGAPI? CHINJA CHINJA WA MAGOGONI ANAWAATUMIA VIBAYA
 
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alishaliona hili siku nyingi......

Alitahadharisha kuwa Katiba yetu inampa nafasi kubwa ya ki- mungu mtu amayepewa madaraka ya Urais!

Akatahadharisha kuwa iwapo nchi yetu itapata kiongozi ambaye "atalewa" madaraka, hii nchi tutakiona cha moto.....

Hii nchi kwa sasa kweli tunakioma cha moto!
 
Aisee mbona wanaaibika sasa, hivi kila kaji kiongozi cha ccm anategemea Naweza mwendesha RPC?
 
Back
Top Bottom