johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,099
- 164,468
Yamekuwepo mawazo chanya baada ya kazi nzuri iliyofanywa na kamati ya Profesa Mruma, kwamba sasa mikataba yote ya madini ipitiwe upya ili kama taifa tujiridhishe na uhalali wake.Sasa wapo wanaosema iundwe tume ya wabobezi wa sheria za mikataba wakaichunguze mikataba hiyo, hawa wanasema kamati ya Profesa Mruma imewatia moyo kwa namna ilibyotimiza jukumu lake hivyo wanapendekeza njia hii itumike tena.Wengine wanasema mikataba ipelekwe bungeni ili wabunge wakaipitie upya, hawa wanasema bunge ndio linawakilisha wananchi ambao ndio wamiliki halali wa rasilimali za nchi hii.Je, wewe mdau unapendekeza nani aichunguze mikataba hii?Karibu kwa mjadala.