Bunge liunde kamati ya kupitia mikataba ya uwekezaji ya kimataifa

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
195
Ni dhahiri kuwa bunge la Tanzania lina wabunge wachache wenye uwezo wa kuchambua mambo na kuleta ujumbe wenye maana.

Pamekuwepo kelele nyingi za kutaka mikataba ya kimataifa kuidhinishwa na bunge kabla ya kusainiwa, lakini je hiyo capacity wanayo? Au wengine ni bendera fuata upepo tu?

Tumeona wakati wa Escrow ilivyokuwa tabu kwa wengine kupata taabu kutengeneza sentensi moja tu yenye maana na mshiko katika masikio ya umma wa Watanzania, je unadhani watu hao wakiletewa mikataba ya kimataifa wanaweza kuiangalia kwa maslahi mapana ya taifa au ndiyo litakuwa janga la kitaifa.

Sikatai kuwa wapo wabunge wenye uwezo mkubwa tu kama wataamua kufanya hivyo, kwa kuzingatia hilo ushauri wangu ni kuwa iundwe kamati ya kibunge ambayo wajumbe wake watachanguliwa kwa kuzingatia uwezo, weledi na uzalendo wa kwa taifa ili iwe kama ya kupitia mikataba husika. Hii itapunguza wapiga porojo ambao wakati mwingine porojo zao zinaweza kukwamisha mijadala yenye afya.
 

mutabilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
305
0
umenena ila nani atakusikia? Nami wa kuchikua hatua hizi? Ili wazo lako zuri ila umechelewa kulitoa na pia ungelitoa katk mapendekezo ya katiba mpya wahusika (CCM) waliokaa bungeni wangeliondoa kwani lisingekuwa na manufaa kwao, lingewanyima ulaji!!!!!!!
Nawasilisha.
 

theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Kweli mdau umeongea point sababu kuna wabunge alipokuwa anachangia suala la escrow mtu anamesoma ripoti zote anazo lakini anachochangia yaani takataka tupu.Kuna yule mbunge Asunta mbunge wa mkenge kama sijakosea pale kwa akili za haraka anaweza kutoa mchango wa kuishauri serekali kweli.Yaani kichwani ni empty set watu wanaongelea Escrow yeye anaongelea habari ya sijui CCM imepanda imeshuka sasa wapo 360's assume type ile wapo 90% hahaha kwanini kusiwepo pumba tupu.Napata wasiwasi na katiba yetu iliyopitishwa na akili za aina ile.Sio kwamba hamna majembe kule yakujenga hoja ila viraza wengi na demokrasia inasema wengi wape.
Tumeshalogwa na aliyetuloga kafa so hata bunge likiunda hizo kamati tunaweza tukaishia tunaishauri serekali ----- zaidi ya uliopo.Dawa ni kutafuta wataalamu nje ya bunge tuwaajiri then bunge ndio likapitie ripoti zao.
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,423
2,000
Watu wengi ambao mnawaita vigogo wana interest kwenye hiyo mikataba.
Subiri tu uje uone au uambiwe. Usikute kwenye ile mikataba lukuki ya naniliu na ............ nae yumo
 

mjuma877

Member
Nov 27, 2014
10
0
umenena ila nani atakusikia? Nami wa kuchikua hatua hizi? Ili wazo lako zuri ila umechelewa kulitoa na pia ungelitoa katk mapendekezo ya katiba mpya wahusika (CCM) waliokaa bungeni wangeliondoa kwani lisingekuwa na manufaa kwao, lingewanyima ulaji!!!!!!!
Nawasilisha.
Mutabilwa na wana JF wengine: napenda niwape taarifa kuwa suala la mikataba kupitiwa na bunge kabla ya kuisainiwa lipo kwenye rasimu ya warioba. Ila kwenye katiba pendekezwa limeondolewa, hii inadhihirisha suala la uwazi kwenye mikataba halijakubalika kwa watawala.Hivyo juhudi za makusudi zinahitajika ili rasilimali za taifa ziwe ni kwa masilahi ya wananchi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom