Kupitia Kipindi cha Chemsha Bongo Radio One nimejifunza kitu

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Jana nimefanikiwa kusikiliza kipindi cha Radio One Chemsha Bongo kuna kitu nimejifunza,kuna maswali ya kawaida tu Yaufahamu zaidi ila wengi waliopiga Simu walikua wakishindwa kuyajibu.

Mfano Jina la Mwanasiasa mkongwe Tanzania kuna mdau alijibu bado halijatokea Tanzania

Malala Ametokea nchi gani huyu dada alitajwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na mateso aliyopitia

Kabla ya Mark Sally Rais wa Senegal aliyepita aliitwa nani,Maswali yote watu walishindwa kuyajibu hadi kufikia Mtangazaji kutoa Majibu.

Taja nchi 3 zinazoanzia na herufi T Afrika Mtu anasema ni Tanzania tu.

Nikajiuliza Je ni Mitaala yetu ya Elimu haiwaruhusu watu kuyajua hayo au?Kipindi cha Nyuma kulikua na Vitabu vizuri sana ya Kiada na Ziada Shule mwetu.

Nakumbuka Jiografia Nimeanza kusoma kuanzia kilimo Cha Buni BUKOBA,Buni BURUNDI Mpaka Buni BRAZIL.

Kilimo cha Ndizi Bukoba,Ndizi visiwa bya Kanali mpaka Ndizi Jamaika.

Jiografia ilikua pana sana kwa leo hii sidhani kama mwanafunzi ukimuuliza kwa Tanzania wapi wanalima Mahindi zaidi atakujibu,Afrika na hata pia Duniani.

Kuna kipindi kulikua na Mashindano ya vyuo Vikuu yalikua yakirushwa Mubashara wenzetu walikua Shapu sana kujibu maswali manake kulikua na Vipengele vya michezo,masomo,historia mbalimbali ila sisi tulikua tunashindwa kuyajibu

Nimeshawahi Kuweka bandiko moja hapa jibu la kwanza watu walinijibu tukishajua itatusaidia nini?niwapongeze walimu wa zamani sana naimani hata sasa bado wapo akikufundisha Jiografia utadhani upo kwenye nchi husika kabisa.

Nliwahi kuwa na Rafiki Mjapan akashangaa nataja timu za kwao za Mpira kama vile Gamba Osaka akashangaa sana ni Sawa leo Umuulize mtu OTELULU GALAT ni timu ya mpira inayotoka nchi gani jibu litakua ili inasaidie nini?

Tupende kujisomea Vitabu mbalimbali ili tujue na Jiografia za wenzetu.
 
Bongo fleva inawaharibu sana watoto wetu (wanafunzi) na hii mitandao ya kijamii (Instagram, Facebook) pamoja na sites za ngono. Mwanafunzi anaenda shuleni kabla ya shule kuanza anaperuzi site ya ngono kwenye simu kuangalia jinsi watu wanavyof.ilana, na kufungua mitandao ya kijamii kujuwa wasanii wa fleva wamekula nini ama kufanya ujiga gani jana.
 
Umeandika kitu kimoja kizuri sana.

Ukitaka uyajue haya angalia kipindi cha Skonga EATV ndio utajua shida iko wapi!

Mwanafunzi wa Kidato cha nne anaulizwa Mkoa Maarufu kwa ulimaji wa Tumbaku anataja "Mkoa wa Songea" .
Kwanza Songea sio Mkoa halafu hawalimi Tumbaku.

Hivi vipindi vinatoa majawabu ya jinsi Elimu yetu ilivyo.
 
Sasa mbona na wewe ni wale wale, Ruvuma hawalimi tumbaku?? ila nakubali kuwa sio maarufu/hawazalishi tumbaku kwa wingi!
 
Akili za watanzania wengi zipo kwenye mambo ya udaku na kufuatilia maisha ya watu ambayo hayana faida yoyote kwa maendeleo ya nchi. Ili uamini hili tafuta wanafunzi kumi wa chuo kikuu halafu waulize maswali yafuatayo; hivi spika wa kwanza wa bunge la Tanganyika anaitwa nani? Nini dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025? Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kina mrengu gani wa kisiasa? Ukiona hayo anababaika sana muulize hivi; hivi wimbo wa kwanza kabisa wa diamond unaitwaje? Kwa Mara ya mwisho, Ali kiba alifanya kolabo na msanii yupi wa nje ya nchi? Eti leo ubuyu wa shilawadu ulikuwa unahusu Nini? Majibu utakayopata sehemu ya pili yatakuwa mujarabu zaidi na pengine sehemu ya kwanza inaweza ikakosa majibu kabisa......
 
Kama think tank wa wasomi wa Tanzania ni Mange Kimambi, unategemea nini??

Vichwa vimejaa ujinga mtupu 24hrs
Bora hata kimambi yeye ana MBA halali kabisa na hakuwahi kughushi chochote!
Sasa mkulu think tank wake na plan master ni bashite, divishen zero asiyejua hata buni ni kitu gani, kwa mtu kama wewe si hohehahe kabisa uliyepo kwenye kundi la profound?
 
Akili za watanzania wengi zipo kwenye mambo ya udaku na kufuatilia maisha ya watu ambayo hayana faida yoyote kwa maendeleo ya nchi. Ili uamini hili tafuta wanafunzi kumi wa chuo kikuu halafu waulize maswali yafuatayo; hivi spika wa kwanza wa bunge la Tanganyika anaitwa nani? Nini dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025? Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kina mrengu gani wa kisiasa? Ukiona hayo anababaika sana muulize hivi; hivi wimbo wa kwanza kabisa wa diamond unaitwaje? Kwa Mara ya mwisho, Ali kiba alifanya kolabo na msanii yupi wa nje ya nchi? Eti leo ubuyu wa shilawadu ulikuwa unahusu Nini? Majibu utakayopata sehemu ya pili yatakuwa mujarabu zaidi na pengine sehemu ya kwanza inaweza ikakosa majibu kabisa......

Japokua mimi si mwanafunzi wala mhitimu wa chuo kikuu (ila kwa umri wangu ningepaswa kuwa miongoni mwao), sehemu ya kwanza ya maswali yako ingenitoa jasho (ningepata swali moja tu la kwanza hayo mengine ningekubabaisha tu) na sehemu ya pili ningeitoa jasho, hiyo sio habari ya kusikitisha (mimi kupata swali moja tu), habari ya kusikitisha ni kwamba eti mimi ni miongoni mwa vijana wanao onekana wana unafuu huku mtaani kwenye suala zima la uelewa. Fikiria hao wengine ninaowashinda...

Tumefikia pabaya, safari ya kujifunza bado ni ndefu sana mbele yetu.
 
Ndipo tujue kuwa sisi bado sana kwenye mambo ya kitaaluma! Ila no matumaini yangu kuwa tukilichukua hili suala na kulifanya kama changamoto huenda tukafika sehemu nzuri zaidi.....
 
Japokua mimi si mwanafunzi wala mhitimu wa chuo kikuu (ila kwa umri wangu ningepaswa kuwa miongoni mwao), sehemu ya kwanza ya maswali yako ingenitoa jasho (ningepata swali moja tu la kwanza hayo mengine ningekubabaisha tu) na sehemu ya pili ningeitoa jasho, hiyo sio habari ya kusikitisha (mimi kupata swali moja tu), habari ya kusikitisha ni kwamba eti mimi ni miongoni mwa vijana wanao onekana wana unafuu huku mtaani kwenye suala zima la uelewa. Fikiria hao wengine ninaowashinda...

Tumefikia pabaya, safari ya kujifunza bado ni ndefu sana mbele yetu.

Uwiiiikweli ww ndo wale wale
 
Soma vizuri nimesema aliulizwa "Mkoa Maarufu unaoongoza" acha ubashite!

Basi sasa, na hapa umeandika nini "Mwanafunzi wa Kidato cha nne anaulizwa Mkoa Maarufu kwa ulimaji wa Tumbaku anataja "Mkoa wa Songea" .
Kwanza Songea sio Mkoa halafu hawalimi Tumbaku."
Hoja yangu hata wewe kwa uelewa wako, mbali na kuwa swali liliuliza mkoa maarufu kwa ulimaji wa tumbako, hujui kuwa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa inayolima tumbaku.
 
Back
Top Bottom