Kupinga kila kitu ni ujinga na hila

jmapunda

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
731
2,922
Awali ya yote niweke wazi kuwa sina maslahi na chama chochote kile cha siasa.

Kwangu Tanzania kwanza. Siku za karibuni kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kupinga kila jambo linalofanywa na serikali bila hata ya kuwa na sababu za msingi. Jamani tupinge kwa haki vinginevyo werevu tutajua labda wanaopinga kila kitu hata kilichochema wana ajenda zao nyingine za gizani.

Jambo jingine la kushangaza kuona baadhi ya watu wanawasikiliza na kuamini kila jambo linalotoka kwa watu hawa. Jamani tuache akili zetu zituamulie badala ya wapotoshaji hawa. Kwa kusema hayo sina maana kuwa naitetea serikali. Hapana. Hata mimi kuna baadhi ya mambo ambayo sikubaliani nayo lakini haina maana nione kila jambo linalofanywa ni baya.

Atakaye kuchangia hapa asituletee mambo ya ma vyama.

Karibu.
 
Ukiona unapingwa kwa kila jambo jirekebishe kuna jambo utakuwa ulikosea. Ukiwa mbaguzi usitegemee kuungwa mkono hata kwa mazuri, ukiwa mpenda sifa basi kila ufanyalo watu watasema ni kiki tu. Ukiwa kiongozi epuka mambo yanayowagawa watu, epuka uonezi na upendeleo ,usipende watu wakujue tabia zako za ndani. Watu wakisha kudharau hata uwaletee pesa watakula na dharau itaendelea tu.
 
Sio kila anayepinga anakuwa na mtazamo hasi mkuu, wengine ni kwa nia ya kurekebisha
 
Back
Top Bottom