Kupimiwa shamba au kiwanja mpaka kupata hati

Kupimiwa shamba au kiwanja mpaka kupata hati

MIkawangu

Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
21
Reaction score
4
Habari wana jamii mwenye kiwanja ambacho hakijapimwa, na anataka kupimiwa mpaka kupata hati, hana muda wa kufanya process za kufatilia wizarani na manispaa wasiliana nasi tunafanya huduma hizo kwa haraka na bei ya kawaida

Wasiliana nasi kwa namba 0712029027
 
Weka bei kulingana na ukubwa.mfano kupima heka 1 ni sh.kadhaa ili mtu ajue kabisa
 
acha kuandka km unakimbizwa wewe, hii issue ni nyeti sana, hebu sema kwa details, uko wapi, na weka makadilio ya bei!
 
Kila mtu na bei yake we mpigie simu tu akusaidie.
 
habari wana jamii mwenye kiwanja ambacho hakijapimwa, na anataka kupimiwa mpaka kupata hati, hana muda wa kufanya process za kufatilia wizarani na munispaa wasiliana nasi tunafanya huduma hizo kwa haraka na bei ya kawaida wasiliana nasi kwa namba 0712029027

Mkuu usikimbie,
Hebu tufafanulie wadau haya maswali ambayo ni general kwanza, kabla ya watu kufanya uamuzi wa kukufatuta. Hii ni biashara ndugu, lazima uwe tayari kutoa maelezo ya kuridhisha clients watarajiwa!!
 
habari wana jamii mwenye kiwanja ambacho hakijapimwa, na anataka kupimiwa mpaka kupata hati, hana muda wa kufanya process za kufatilia wizarani na munispaa wasiliana nasi tunafanya huduma hizo kwa haraka na bei ya kawaida wasiliana nasi kwa namba 0712029027
Mkewangu hembu fafanua vizuri,hii issue watu wapo wengi wanakwepa usumbufu.
Weka mchanganuo wa mfano
 
okey hii ishu ipo hivi, kama una ardhi haijapimwa kwanza tutatakiwa tuiangalie kwa kuchukua coordinate za eneo husika na kuzipeleka ARDHI, hapo watatuangalizia eneo letu kama lina mchoro au halina mchoro. kama Eneo lina mchoro tutaangalia eneo hilo ni la matumizi gani? kama ni matumizi sahihi tutaanza process za kupima.

kama eneo lako halina mchoro tunakuandalia mchoro tunaupeleka manispaa husika ukipitishwa tunaurudisha ardhi kwa process zingine, kwa kesi hii ya ardhi isiyo na mchoro kidogo pana shida kama kiwanja kipo kimoja hasa hapo kwenye kuupitisha manispaa

baada ya kupata mchoro na kujiridhisha na matumizi ndo tunaanza kazi ya survey mpaka kupata offer then kupatikana kwa hati.
kama unahitaji tukakuangalizia eneo tu gharama zetu ni laki 3
kama ulishaanza umefika hatua ya kuweka mawe huna hati tukianzia kwenye mawe mpaka hati gharama zetu ni milion 2
na kama unataka tukufanyie kazi kanzia kuangalia eneo hadi kukupimia namaanisha kuweka mawe gharama zetu ni milion 2
na kama unataka tukufanyie mchakato mzima gharama zetu ni milion 4
karibuni
 
Kuangalia eneo tu laki 3 sasa kama najuwa eneo langu lipoje na mchoro ninao je mna haja ya kuangalia??
 
Ekari kumi mkuu maana naona jamaa mwenyeewe anaandika kkitu bila kuwa na details kamili

Asante, let's assume mchoro upo nahitaji kupanda mawe ktk eneo la ekari 30, ambalo lote lina viwanja vya robo ekari gharama itakuwaje?
 
Duh kweli ujinga ni gharama sana, kuangalia eneo ni laki 3? Yani kupata mchoro wa jiji na kuchukua Gps na kwenda eneo husika 300,000? Mmh
 
Duh kweli ujinga ni gharama sana, kuangalia eneo ni laki 3? Yani kupata mchoro wa jiji na kuchukua Gps na kwenda eneo husika 300,000? Mmh

Bro we are all born ignorant, hii si dhambi, dhambi ni kutokuukana huo ujinga kwa kutafuta maarifa, elimu na kweli, nakuomba utusaidie kutupa facts za gharama halisi, utakuwa umetutendea haki sisi waja wa Allah, nawe utaipata thawabu
 
Huhitaji kugharamia kujua plot yako kama imepimwa ama la. Hujui Global Position System (GPS)? Basi utaendele kuibiwa tupu, hiyo ni elimu ya basic kbs, gps ziko mpk za laki tu na simu zingine ziko nayo.
Afu punguza maneno ya kiswahili swahili
 
Asante, tupunguzie usumbufu, tuelekeze pahali sahihi
 
Duh kweli ujinga ni gharama sana, kuangalia eneo ni laki 3? Yani kupata mchoro wa jiji na kuchukua Gps na kwenda eneo husika 300,000? Mmh

Ndio hapo sijaelewa labda aje afafanue vizuri inakuwaje kwenye hiyo laki 3???maana naona kuna changa la macho hapo.... xfactor tafadhali njoo mara moja tusaidie hapa.....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom