Wakati unapoenda kupima maambukizi ya ukimwi hospital kinachopimwa ni antibodies. Hizi ni 'kinga' inayotengenezwa na mwili wako kama jibu ya mashambulizi ya virusi vya ukimwi. Hizi antibodies zinaweza kuchukua muda kuonekana kutegemeana na kwamba virusi vimejificha wapi. Huwa hatupimwi kile kirusi chenyewe unless umeenda kupimwa DBS/PCR ambayo huwa inapima DNA ya virusi.
Hii DNA ya virus huwa inapimwa hospital kuu nne Tanzania Muhi2, Bugando, Mbeya referral na KCMC ila ni special kwa ajili ya watoto tu na huwa wanapimwa wanapofikisha mwezi mmoja. Sisi wengine wote huwa tunapimwa na Determine na Unigold ambazo zinacheck antibodies and therefore you just need to wait for the three months to confirm status yako ya maambukizi.
Hope I have shed some light on your issue.