Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,287
- 10,839
Wana JF,
Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya Ukimwi Duniani na Tanzania tunaungana na dunia kusheherekea siku hiyo. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni pamoja na kupunguza vifo, maambukizi mapya na unyanyapaa!! (nimechukua key words tu). Ukiangalia maongezi mengi kila mtu anasisitiza upande wa maambukizi mapya ni shurti kuwa na mpenzi mmoja mliyepima na kukuta mko safi na hakuna pepesa pepesa tena nje, ya pili ni kutumia kondomu. Hili la kondomu bado nina tabu nalo kwa sababu kuna watu wameambukizwa virusi na huku walitumia kondomu. Hii inawezekana kutotumia kondomu kwa usahihi lakini pia kuna wengine kondomu zinapasuka ndani ya game!! Sasa ninashauri kuwe na vipimo vya haraka ambavyo vinaweza kuonesha virusi vya ukimwi kwa mtu kabla ya miezi mitatu wanayosema wataalam ili ukikutana na aliyekuzingua basi hapo hapo mpelekane kwa pilato mkapimane ili angalao kama kondom itapasuka usipate madhara. Hili suala la kupima halafu uambiwe urudi baada ya miezi 3 maana kama mtu umepata virusi leo au mwezi uliopita na haviwezi oneekana kwa vipimo vyetu ni hatari sana. Ila pia nasikia kuna hospital Tanzania ambazo huwa zina vipimo sensitive ambavyo vina uwezo wa kuona virusi hata cha mwezi mmoja!! Kwa nchi za wenzetu nasikia vipo na vimeokoa wengi. Kwa kuwasaidiana hapa je hapa Tanzania kuna hizo hospital ambazo unaweza kupima virusi vikaonekana kabla ya miezi mitatu? Kama zipo ni zipi? Na bei yake ni kiasi gani? Tafadhali toa maoni au majibu ya kuwasaidia watu hapa ikiwemo na wewe maana hapa tunapeana elimu pia. Post za kejeli hazitafurahiwa. Asante na karibuni kuelimishana.