Kupiga mruzi kuna kasoro gani?

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
Jana nilikuwa kwenye lift za jengo la PPF Tower. Mara nyingi nina tabia ya kupenda kuimba au kupiga mruzi hata ninapokuwa mwenyewe au hata niapotembea.

Lakini ninapkuwa kwenue public basi hata kama napiga mruzi huwa nahakikisha kuwa sauti inayotoka ni ndogo ili isikere walio karibu yangu. Ndivyo jana kwenye lift nilivyokuwa napiga mzuri.

Mbele yangu akawepo jamaa mmoja aliyeaamua kunieleza kuwa nisipende tabia ya kupiga mruzi kwenye public. Mimi nikauliza sababu yake ni nini maana mruzi wangu hauleti kelele kama yale mazungumzo.

Akasema unapopiga mruzi unatoa hewa mdomoni ambayo inaweza kumfikia mwingine na kama una maradhi basi uambukizaji ni rahisi!

Hata wenzangu bado walishtuka na sababu hii na alivyoona tunashtuka akasema ana uhakika na anachokisema kwa sababu yeye ni daktari.

Mimi nikazidi kumbana kwa kumuuliza, mbona tunapoongea hewa ni ileile inayotoka mdomoni na inasambaa kwa majirani?

Akaeleza kuwa hewa inayotoka kwa mruzi ni nyingi kuliko ile ya kuongea! Wakati anajibu hivi akawa anashuka alipofika sisi tukawa tunaendelea floor zilizofuata. Mmoja wetu akamjibu "Asante kwa elimu" kwa maana ameelimika.

Lakini mimi sikuishia na elimu ile tu. Kwa nileiendelea kujiuliza mbona vitendo vya kutoa hewa ni vingi tu kama vile kucheka nk.

Kama kuna madaktari hapa JF au hata wenye uelewa zaidi tuelimishane ukweli wa nilichoeleza. Kwani binafsi sina data za kujua hewa ya maongezi inatoka kwa rate gani na hewa ya mruzi au kucheka inatoka kwa rate gani.
 
Back
Top Bottom