Kupiga hatua katika biashara yako

gema

Member
May 26, 2011
25
20
Unaweza soma makala nyingine nyingi za uwekezaji na ujasiriamali kwenye tovuti ifuatayo: Uwekezaji na Ujasiriamal(Bofya Hapa)

Hatua ni umbali kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine au kutoka kiwango kimoja kwenda kiwango kingine. Mtu ambaye hapigi hatua katika biashara yake ni mtu ambaye yuko kwenye kiwango kimoja tu cha biashara kwa kipindi cha muda mrefu.

Mtu anapokuwa anapanda ngazi au kushuka ni lazima apige hatua moja ikifuatiwa na hatua nyingine na kadri atakavyokuwa akiendelea ndivyo atakuwa akiikaribia hatima yake au mahali alipotakiwa kufika. Hatua kwenye biashara ni mfano wa ngazi hivyo unapaswa kupiga hatua moja kwenda nyingine ili uweze kufikia hatima yako.

Katika biashara kuna watu aina tatu.

(i) Watu ambao hupiga hatua kwenda mbele mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wenye thamani ya shilling 1,000,000 mwaka huu ameongeza mtaji wake kufikia thamani ya shilingi 1,500,000.

(ii) Watu ambao hawapigi hatua kabisa mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wenye thamani ya 500,000 na mwaka huu thamani ya mtaji wake ni shilingi 500,000.

(iii) Watu ambao wanapiga hatua kurudi nyuma mfano mwaka jana alikuwa na mtaji wa shilingi 1,000,000 lakini mwaka huu mtaji wake umepungua thamani kufikia shilingi 700,000.

Kila kitu katika maisha kina hatua ambazo kinapaswa kupitia ilikufikia katika utimilifu wake hata mwadanamu kuna hatua mbalimbali za ukuaji ambazo anapaswa kupitia kutoka utoto mpaka utuzima. Mtoto anapokaa kwenye hatua moja ya ukuaji kwa kipindi kirefu huwa tunasema mtoto huyo amedumaa, biashara inapokaa katika hatua moja kwa kipindi kirefu biashara hiyo husemekana ya kuwa imedumaa au haiendelei, mti wa matunda unapokaa muda mrefu bila kuzaa huwa tunasema mti huo umedumaa au haupigi hatua.

Kama unahitaji kuwa na uwekezaji au biashara yenye tija ni vema swala la kupiga hatua ukalipa thamani kubwa kwasababu ndio linakueleza kama biashara yako inakuwa au la. Thamani ya mtaji wako iko ndani ya muda hivyo endapo hautajifunza kufanya vitu ambavyo vitakusaidia kupiga hatua huenda baada ya muda ukiangalia thamani ya mtaji wako utakuta umeshuka thamani kwa kiwango kikubwa.

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo yanaweza kupelekea biashara yako kutopiga hatua stahiki mfano kutokuwa na mpango kazi katika biashara , kukosa vipaumbele katika biashara yako, kutopenda kujifunza mambo mapya ambaye yataongeza thamani katika biashara yako , kutofanya thamini ya biashara yako, Kuwa na mipango mizuri isiyokuwa na utekelezaji na kuzikimbia changamoto badala ya kuzikabili. Jambo baya unapokimbia changamoto ni kwamba hautajifunza nini chakufanya na pia kuna uwezekano wa changamoto hiyohiyo kujirudia lakini unapokabiliana na changamoto itakusaidia nini chakufanya na kuweka mpango mkakati wa kukabiliana nayo mapema ( proactive strategy).

Ni muhimu sana kupiga hatua katika biashara yako maisha ili kuweza kufikia hatima yako na kuwa mtu mwenye furaha. Fanya tathimini ya kina katika bishara yako ili kujua kama unapiga hatua au la na kisha weka mpango mkakati wa kuhakikisha unapiga hatua vema ili kufikia hatima yako.

Imeandaliwa na
James Albert
2016

Unaweza soma makala nyingine nyingi za uwekezaji na ujasiriamali kwenye tovuti ifuatayo: Uwekezaji na Ujasiriamal(Bofya Hapa)


 
Back
Top Bottom