Kupendwa ndo Huku sasa

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,012
71,167
Mida fulan nimetoka kupata huduma Duka jirani hapa.

Sasa wakat natembea Mbele yangu alikuapo Mdada mmoja na wamama wawili wanatembea wakipiga stori


Haka kadada kiumri ana miaka 20-25 ,inaonekana walikua wanatoka kwenye mishe zao ..


Sasa wakakutana na Binti wa miaka kama 13 ivi..

Kadada kamuuliza, Mwanangu mmemlisha chakula??


Kale katoto kakamwambia, Badoo ...

Haka kadada kakawambia wale wamama,

"Daahhh Jamaani huyo mtoto ni kila kitu kwangu, nampenda kuliko kitu chochote ,naposikia habari kama hizi, nahisi nataka kufaa, ebu tuongeze mwendo "


Mmoja wa wale wamama akamjibu..." Mpende mwanangu ,wee mpende mwanao, ndo maisha yako, mpende sana ""...


kilichofanya nikatabasam ni yale maneno ya kale kadasa kuhusu mwanawee

Hivi kumbe MAMA ZETU WANATUPENDA NAMNA HII???..

Alafu unakuta mtu anamdharau mama yake, anamtukana hata kumpiga?? Kweli ?? Kwamba baada ya kufanikiwa maisha, tunawasahau hadi Mama zetu!!??



Sisi ambao Mama zetu bado wapo hai, Tuwapende sana mama zetu.
 
Madingi tuna nafasi kubwa sana ya kuwashepu watoto mkuu. Kwa jinsi wamama wanavyopenda watoto wao, kama sio sisi watoto wangeharibika kabisa maana mama zao hua hawawezi kufanya chochote kwa watoto.
I appreciate madingi tupo gud japo wanavunga hawatuoni..
 
Ila mimi huenda napenda ngono sana.

Yaani nilivyo ona kichwa cha habari cha hivyo nikajua ule upendo common nimewahi kuja kusoma najua mwisho utafunua uzi pendwa wa rikiboy
 
Back
Top Bottom