Kupenda kunaumiza

tetestaly

Senior Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
126
Reaction score
59
Nilikuwa na mpenzi niliyempenda sana , ila juzi nilimpigia simu akadai yuko kazini akaniambia akitoka ataniambia. Baada kama masaa mawili akanipigia simu akaniambia tukutane mahali fulani muda fulani nikamjibu sawa , baada kama lisaa limoja tena akatuma text akisema bby tuonane kesho, nikajibu ok kwa shingo upande mimi nikarudi nyumbani na usiku ulikuwa umeingia.

Badae nikapiga simu yake haipatikani , nikatuma txt nahisi unanicheat kwanini unizimie simu? ok me nikaingia kulala.

Saa tisa usiku nikapigiwa simu kupitia simu ile ya mtu wangu ila aliyeongea sio yeye aliongea mtu jinsia sawa na mimi kwa kutumia simu ya mtu wangu akiniuliza we ni nani unayemtumia mtu wangu txt nikamjibu muulize huyo uliyenaye mimi ni nani kwake. Sikuweza kuongea kwa ukali maana nilikuwa na mtu jilani yangu (ndugu yangu ambaye nalala naye chumba kimoja) akakata simu.

Nikatoka nje ili ni mpigie niongee naye huyo mtu aliyenipigia simu kupitia simu ya mtu wangu ile simu hakupatikana tena, mchana akanipigia huyo mtu wangu sikuweza kupokea maana nilikuwa na hasira sana akatuma txt ya KUOMBA msamaha sikujibu chochote , leo nimempigia simu nikimuomba tukutane sehemu flani ila hajaja baada ya mimi kuondoka anapiga simu nikasema nimeondoka akasema poa.

Naombeni ushauri wakuu na mimi nijifanye mjinga nimsamehe ili nami nilipize kisasi au nimsamehe tu niendelee naye au nimpige chini niachane naye kabisa? Au wewe unashauri nini?
 
Kwenye mapenzi kuna mawili yatatokea kuumizwa ama kuumiza. Lakini ukijitia unataka kulipiza kisasi ni sawa na mbuzi aliefia kwa muuza supu utachinjwa bila ya kupiga kelele. Juu ya uchepukaji wangu lakini sijawahi kumpatia mwanamke mwengine aongee na mchepuko wangu. Siku ya ukame mchepuko utakuja kunisave tu.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
I beg to those who died long ago
Those who died in accidents
Those who died with malaria
Those who died because of war
Those who killed themselves because of money
To ask God
since they are next to him
If He could reduce the pain of those suffering because of love
Since he says that He is Love
yes God is love, God is love
Even a virus has an antidote which is an antivirus,
But the guy who invented love didn't give us instructions
That's why we were expecting for Jesus to come on Earth and teach us so we can see how it works
But unfortunately Lord Jesus had no girlfriend
That's why we're blindfold,
That's why we keep trying and struggling,
Sometimes it goes well and sometimes not at all



Mkuu hiyo ni mistari ya nyimbo ya fally ipupa -bruce
Ushauri wangu kwako achana na mapenzi just work hard,utakuja pata ukimwi bule papuchi sio ya kushare

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole naamini yajayo hutokuja kuomba ushauri,fuata nini dhamira ya moyo wako inataka
 
Kisasi hutakatisha nafsi. Usimwache hivihivi. Mfanyie kitu kibaya ili ajue ulivyojiskia maana ukimwacha hvyohvyo atajua ulichukulia poa coz na ww ulkuwavunacheat.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama utaridhia ku-share mwanaume ,it's ok endelea nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imeandikwa malipo ni hapa hapa duniani. Ni mapema mno kumuacha huyo msaliti. Jifanye mjinga when you get a chance mpe kisasi anachostahili ili aelewe alichokuwa anakufanyia wewe sio kitu kizuri.
 
Mpaka hapo kipi usichokijua?? Usipingane na ukweli ukabili mwache aende si uliepangiwa huyo
 
ushasema unampendaaa utakaaa nae ili umfanyie hataa asiumie utaishia umia ww....ukiachwa achikaa dada
 
kutana nae kwanza umsikilize atakachosema alaf utajua cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…