Kupeleka wanafunzi Harvard, kufuta tozo ya VRF na kuongeza fedha ya kujikimu kumeacha alama isiyofutika kwa watanzania, asante Rais Samia

Kupeleka wanafunzi Harvard, kufuta tozo ya VRF na kuongeza fedha ya kujikimu kumeacha alama isiyofutika kwa watanzania, asante Rais Samia

msuyaeric

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
862
Reaction score
1,249
Na Mwl. Udadis, Mazimbu

Value Retention Fee (VRF) kwa lugha ya Kiswahili ni tozo ya kutunza thamani ya fedha (mkopo). Kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, kila mmoja alikuwa akilipa 6% ya deni kama VRF, jambo lililokuwa likiumiza wanufaika. Kitendo cha Rais Samia kuamua kufuta tozo hii kumetoa fursa kwa wanufaika wa Bodi kutumia fedha hii kwa mambo yao ya msingi, na hivyo kuondoa mzigo uliokuwepo. Hii ni alama isiyofutika mioyoni mwa wanufaika.

Kwa muda mrefu, wanafunzi wa elimu ya juu walikuwa wakipokea Shs 7,500 kama fedha ya kujikimu kwa siku. Ili kuboresha maisha ya wanafunzi hawa, Rais Samia aliamua kuongeza kiwango hiki na kuwa Shs 10,000 kwa siku ili kuwapa wanafunzi urahisi wa maisha na fursa ya kujikita kwenye masomo kwa ufanisi zaidi. Hii ni alama itakayodumu mioyoni mwa vijana, hasa wasomi wa vyuo vikuu.

Katika kipindi cha miaka minne, bajeti ya mikopo ya elimu imepanda kutoka Shs bilioni 464 (2020/2021) hadi Shs bilioni 786 (2024/2025), sawa na ongezeko la 69.4%. Hii tafsiri yake ni kwamba kila mwenye sifa ya kupata mkopo anaupata bila shida, ili aweze kufikia ndoto zake za kitaaluma. Hii imeacha alama ya kipekee, hasa kwa vijana wanaotoka katika familia zenye kipato kidogo.

Licha ya ongezeko kwa wanufaika wa mikopo na kiwango cha mikopo yenyewe, pia katika kipindi cha miaka minne, Rais Samia ameanzisha 'Samia Scholarship' ambapo wanafunzi wanaopata ufaulu wa juu katika masomo ya Sayansi husomeshwa bure. Na kwa mwaka huu, waliofanya vizuri zaidi wanaenda kusomeshwa katika vyuo vikuu bora duniani vilivyopo Marekani na Uchina. Hii ni alama itakayobaki kwa vizazi vingi vinavyokuja.

Bado sijaeleza Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi ambao wamepata udhamini wa kwenda kunoa bongo zao huko ughaibuni. Uwekezaji huu unalenga kuhakikisha magonjwa yanayohitaji wataalam wabobezi yanatibika hapa nchini na si kwenda Apollo India. Hii ni Alama itakayodumu mioyoni mwa kila mtanzania bila kujali itikadi. Ndio maana watanzania wengi tunasema tunalo deni kwa Rais Samia na tutalilipa kwa upendo Mwezi Octoba. Asante Mama kwa huduma!
 
Kwa hili mama aliupiga mwingi sana. Kwakweli mwendazake#£#%&%£#
 
Back
Top Bottom