Kupata kazi kweli kazi!

Kupata kazi kweli kazi!

king khalfan

Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
70
Reaction score
21
Habari zenu bandugu!? Hivi ugumu wa kupata ajira iwe serikalini au private sectors ni kutokana na mfumo mbovu kuanzia wa elimu hadi waajiri wenyewe au ndo masuala ya kujuana na udugu? Uliye na kazi chapa kazi kwn kupata kazi ni kazi nyingine. Nawaclisha
 
Pole hilo nalo litapita,vumilia usikate tamaa.
 
Umenikuna na Thread yako. Ila nadhani tatizo kubwa ni mfumo uliyopo, umeoza na sasa unanuka na zaidi takribani 80% imefanywa kuozeshwa na serikali ya awamu ya 4 hii. Yaani kupata kazi eti lazma awepo wa kukushika mkono. Eti, ninavyosikia hata rushwa yenyewe mpaka awepo atakayekudhamini kupokea rushwa hiyo lasivyo napo hupati. Kwa kweli inavunja moyo sana. NADHANI WANJIFANYA KUTIMIZA UNABII WA YESU KATIKA BIBLIA TAKATIFU KUWA "ALIYE NACHO NDIYE ATAONGEZEWA" yaani hii nchi inaonekana yaa watu fulani na siyo watz wote. Namuomba MUNGU Atupigania vita hii.
 
Yaani balaa juu ya balaa tu. Elimu yenyewe tumekopeshwa then na kazi wanataka tununue, duuh! Ndo maana hakuna tija, ufanisi, wala weledi unaohitajika ktk kazi hakuna tena. Ofisi nyingi zimejaa urasimu na ubabaishaji kwa sababu hakuna tena nidhamu ya kazi. Utahoji nini wakati mfanyakazi kainunua kazi, au kashikwa mkono na mtu mzito ktk ofc. Hali hii hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu, hivyo hawa watu jamii ya naibu waziri wa elimu wapo wengi ktk sehemu nyeti na muhimu za serikali zenye kuhitaji weledi mkubwa. Anyway tutafika tu hata kwa kujikongoja
 
Back
Top Bottom