BUCHANAGANDE
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 1,512
- 482
Jwtz Wangetoa ajira ili tupungue mtaani kabla ya 2015 ili ccm ipate vikura flani hivi.
Hii nayo Kaali. Kujaza majenerali nako ni janga tuu. kama kweli hawatakuwa na kazi, si mnajua wasiokuwa na kazi wanakuwa ni workshop ya shetani. Hii naweza kusema ni tatizo la ki sera na mikakati. kama career planning iko kizungumkuti, basi inafikia tu wapewe ma vyeo hayo. Huwezi kuendelea kukaa na kuwaangalia disgruntled colonels, japo nayo hiyo si suluhisho. mlolongo wa kupandisha vyeo utaendelea to hadi cheo cha mwisho kabisa chini. Majeshi mengine yalishaliona hilo na wakaweka msimamo wa kuwa muundo siku zote utasimamimiwa bila kufinya macho. Merits na nafasi zitatumika. Sasa, kama wengi wanazosifa basi huitwa na kuelezwa wako over due, lakini hawatavaa manyota, bali watalipwa kiwango cha cheo hicho. baada ya muda kama hawakupandishwa vyeo wanastaafishwa na kulipwa haki zao zote. hii husababisha system/jeshi kupumua. bila hivyo. ni kuahirisha tatizo.
gabriel sanya,Takribani miaka minne iliyo pita upandishwaji vyeo vya maafisa wakuu ( Brig Gen )umekuwa ukifanyika bila kufuata !!MUUNDO WA JWTZ'' Muundo kwa maana ya ukubwa wa jeshi idadi ya nguvu kazi iliyopo, ikijumuisha askari na silaha.
Tafsiri iliyopo inaonekana vyeo vinatolewa kama zawadi na sio kwa kufuata Merits. Inashangaza kuona jeshi linakuwa na majenerali wengi ambao hawafiti kwenye muundo., athari zake ni serikali kujibebesha Mzigo wa fadhila uchwara. Baadhi au wengi wao wanaishi kwenye nyumbani za kupanga uswahilini ambazo pengine hazina hadhi ya chao chake na huenda pia hazipo katika maeneo yenye usalama. Kwa maana nyingine watahitaji nyumba zilizo kwenye maeneo salama.
Tutafakri !!!!
Jwtz Wangetoa ajira ili tupungue mtaani kabla ya 2015 ili ccm ipate vikura flani hivi.
gabriel sanya,
madai kwamba askari wanapewa vyeo kama fadhila(Rejea kwenye RED) ni tuhuma mzito hasa kwa kuzingatia unyeti wa taasisi husika (jeshi). Kusema kwamba wanapewa vyeo kwa fadhila ni sawa na kusema kinachofanywa na Ikulu na washauri wake ni kuingiza siasa, undugu, uswahiba na mambo mengine kama hayo kwenye jeshi letu.
Sasa basi, hebu rejea hapo kwenye BLUE na RED kisha u-connect dots ili kutia nguvu hoja yako. Maelezo yako yanaelekeza kwamba upandishwaji wa vyeo jeshini ni lazima uendane na muundo wa JWTZ, Muundo kwa maana ya ukubwa wa jeshi idadi ya nguvu kazi iliyopo, ikijumuisha askari na silaha. Now questions:
- Jeshi letu ni kubwa kiasi gani ili tujiridhishe kwamba upandishwaji wa vyeo haukuzingatia kigezo hicho?
- Idadi ya nguvukazi iliyopo jeshini ni kubwa kiasi gani in terms of askari na silaha?
- What's acceptable proportional(as per TPDF) kati ya Muundo wa Jeshi na Maafisa Wakubwa wa Jeshi?
- What kind of acceptable merits for one to be promoted? Elimu? Muda aliokaa jeshini? Mtulinga? Nidhamu? Or what really?
- Basing on the question above, ni nani na nani unaamini haku-meet TPDF's acceptable merits?
Kama huna majibu ya hayo maswali, basi tuyaache haya masuala ya kijeshi na usalama kwenye siasa zetu. Nasema hivyo coz' ingawaje mimi si mwanajeshi, lakini nafahamu wazi kwamba JK hawezi tu kuamka asubuhi na kuunda vyeo vipya na kuvigawa kwa watu wake bila kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa masuala ya kijeshi. Ukiangalia kwa makini, utaona hata kwenye jeshi la polisi kuna kuongezeka kwa idadi ya Makamishina tofauti na zamani. Akili ya kawaida, inashawishi kwamba kuna restructuring inafanyika kwenye majeshi yetu; na sio lazima wala salama kuita media na kutangaza kwamba wanafanya restructuring kwenye majeshi yetu.
Nimemsoma East African Eagle, nimemuelewa sana! Tena kwa maoni yangu, pamoja na EAE kusema wanakuwa attached na wazoefu kwa muda mrefu ili wapate uzoefu zaidi; binafsi naweza kuongeza kwamba wanakuwa attached na wazoefu ili wapate pia kuwasoma coz' they're about to be operative in sensitive posts! Unapokuwa karibu na mtu for as many as five years, ni rahisi pia kumfahamu kiundani where he stands linapokuja suala zima la usalama wa nchi hii!
Lakini mwisho nimalizie tu kwa kusema kwamba, si busara kuleta tetesi kwenye masuala ya kijeshi hususani tetesi hizo zinapotoa muelekeo wa kuwapo discrimination jeshini. Kudai kwamba vyeo vinatolewa kwa upendeleo ni kusema kwamba kuna discrimination linapokuja suala zima la utoaji wa vyeo. Na ikiwa kuna watu wanapewa vyeo kama fadhila bila kujali merits, hii ni sawa na kusema kwamba wapo pia wenye sifa za kupata vyeo lakini hawapewi kwavile hawapo within the circle.
Mkuu gabriel sanya heshima sana,
Rais Kikwete ni amiri jeshi mkuu kwa mujibu wa katibu ya JMT anayo mamlaka kamili ya kupandisha cheo wanajeshi.Mpaka hapo sioni kosa alililofanya.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali Tanzania inakisiwa kuwa na idadi ya wanajeshi (active personnel) 27,000 - 30,000 tu.Tanzania pia inakisiwa kuwa na jeshi la akiba (reserve personnel) 80,000 - 100,000 tu hawa ni wale waliopitia jeshi la mgambo,JKT na askari wastaafu wenye nguvu.
Ukubwa wa jeshi ni kigezo muhimu sana unapotaka kupandisha vyeo askari.Kigezo kingine ni uwezo wa kiuchumi pia uangaliwa sana.Kama uchumi wako si mzuri sana kuweza kuhimili matumizi yasiyoweza kuepukwa kama mishahara inayokidhi mahitaji muhimu,vifaa vya kisasa na nk.Kigezo kingine ni hali ya usalama,ikiwa nchi iko katika hali yakuweza kuvamiwa ni lazima bajeti iongezeke mara dufu hapa nazungumzia vifaa na kuongeza idadi ya wanajeshi.
Ukiangalia idadi ya wanajeshi wetu na idadi ya mageneral haziendani hata kidogo, unapokuwa na Lt General 4. kama kumbukumbu zangu ziko sana kuna mkuu wa utawala jeshini Lt Gen S Ndomba, kuna Lt Gen mwingine yuko ofisi ya waziri mkuu (maafa) kuna Lt Gen Mwingine ni mkuu wa chuo cha taifa cha ulinzi kuna mwingine sikumbuki akapachikwa wapi.Ukienda kwa Major General labda sasa wanaweza kufikia 20 ukishuka ngazi ya Brig General wanaweza kufikia 50 au zaidi.Mfano chief of personnel ni Major General na director wake ni Major General.Ukijakutazama idadi ya Brig General utakuta wengi hawana kazi zinazoendeana na majukumu yao sana sana utakumbana na siasa mtindo mmoja
Bila shaka yule aliyekuwa kwa Bwana Mkubwa hajafurahia hicho cheo kwa mwaka huu, pengine ingelikuwa mwaka kesho baada ya kuwa wameshazunguka duniani kuaga. Mafao ya kuzunguka ughaibuni sidhani yanalingana na yale ya kuketi pale Ngome. Pengine angeulizwa kabla, angeshauri abaki hapo hapo na cheo kile kile cha awali hadi Oktoba 2015! ni mtazamo tu!