Kupandishwa kwa nauli

Kupandishwa kwa nauli

Truly

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
228
Reaction score
32
Watanzania wa kipato cha chini mbona mambo yanazidi kutuendea kombo! Nauli mpya zaja , mgao wa umeme ndo kwanza umeshika kasi, umeme wenyewe bei juu mambo kibao bei juu. Wenye nyumba nao kupandisha bei kila mwaka. Maji yanatoka mara moja kwa mwezi bili nayo ulipe. Yarabi toba mtanzania mimi maisha bora kwa kila mtz hakuna.
 
jamani watanzania hebu tuaznze maandamano kuanzia tar 29 feb
 
Watanzania wa kipato cha chini mbona mambo yanazidi kutuendea kombo! Nauli mpya zaja , mgao wa umeme ndo kwanza umeshika kasi, umeme wenyewe bei juu mambo kibao bei juu. Wenye nyumba nao kupandisha bei kila mwaka. Maji yanatoka mara moja kwa mwezi bili nayo ulipe. Yarabi toba mtanzania mimi maisha bora kwa kila mtz hakuna.

suluhisho ni rahisi tu
Nendeni barabarani kama walivyofanya Tunisia, Egypt, kama huo uthubutu haupo ni bora mkaendelea kufa na tai shingoni
 
nauli za mabasi mikoani zimepaaa kwa kila class ya basi imeongezwa 3000, ordinary kama ni dar mbeya ilikua 24 sasa ni 27 semi luxury itakua 30000 na luxury 33000, same applied to kaskazini, central, yaani ni kwa tanzania nzima. wakat mishahara yetu ipo palepale, mi naona watasafiri wenyewe , hawa watu wapuuzi kweli kweli hawatujali walalahoi wenyewe wna maVX na wengine wanapanda bure kwenye mabasi hwana uchungu kabisa na sis
 
maisha yanapanda kwa asi zaidi,nguvu zaidi na hali zaidi.....................
 
na bado!

natamani petroli ifike sh 3800 kwa lita, mfumuko wa bei asilimia 25 au zaidi, nauli iwe hata buku mbili kwa trip halafu nione kama mtakubali tena kura zetu kuchakachuliwa kirahisi namna ile
 
bado za daladala, mtakoma mwaka huu, ah ila nilisahau, sisi lakini tuna amani na utulivu, vinatutosha !
 
Tuleni tu, endeleeni kuvumilia hadi miaka mitano ipite ndo muamue kusuka au kunyoa!
 
dah,
halafu serikal ilitaka nikafanye kaz kigoma,ningerudije?
 
Ndio tunaanza sasa maisha bora kwa kasi zaidi, ari zaidi na nguvu zaidi.
 
bado za daladala, mtakoma mwaka huu, ah ila nilisahau, sisi lakini tuna amani na utulivu, vinatutosha !
aaaaaaha watu hawana utulivu na amani moyoni,hapa nikumkataa rais na serikali yake tu
 
Muda si mrefu tutakuwa na wakimbizi watakaokimbia nchi kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu!
 
Bado watanzania tunaweza kumudu gharama za maisha, siku tukishindwa tutadai haki yetu. Au mnaonaje wkauu?
 
Back
Top Bottom