Kupanda na kushuka kwa simu za Nokia

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Je, unaikumbuka siku za Nokia na enzi zake? Jina Nokia linatokana na mji mdogo nchini Finland, ambapo simu hiyo iliyokuwa maarufu duniani iligunduliwa.

Kwa sasa kuna ishara ndogo kuwa mji huo mtulivu wakati mmoja uliipa simu jina lake, simu ambayo ilibadili kabisa sekta ya simu mapema miaka ya tisini na kubadilisha kabisa uchumi wa Finland kuufanya kuwa uchumi ulioboreka kwa haraka zaidi duniani.

Wakati ikiwa katika kilele chake kwa mapema miaka ya 2000, Nokia iliuza asilimia 40 ya simu zote duniani ambapo ilitambuliwa na kuwa simu maarufu zaidi duniani.

160318142506_nokiagofigure3.jpg

Nchini Finland kwenyewe matokeo yalikuwa hata makubwa. Kulingana na taasisi inayofuatilia uchumi wa Finland ni kuwa simu za Nokia zilichangia robo ya uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 1998 na 2007.

Wakati wa kilele chake, iliwaajiri zaidi ya watu 4,000.

Lakini kwa ghafla soko la simu za Nokia lilishuka kwa kishindo na mauzo kudorora kabisa hali hiyo iliathiri pakubwa uchumi wa Finland na pia kusabibisha kuwepo kipindi kigumu na kirefu kwa uchumi wa nchi hiyo.

"Nokia ilikuwa ni uti wa mgongo wa kila kitu hapa, kuanguka kwake ilikuwa ni kama jinamizi kwa taifa la Finland kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchumi na maendeleo ya mji wa Tampere, Kari Kankaala, mji ulio umbali kidogo kutoka Nokia.

Nokia iliathiriwa sana na kubadilika kwa teknolojia ya simu.

Ilijipata katika njia panda hasa kutokana na kutokea kwa simu aina ya smartphone, na hasa kuzinduliwa kwa simu ya iPhone na kampuni ya Apple mwaka 2007.

Meneja wa zamani wa utafiti wa ustawi katika Nokia Mika Grundstrom anasema kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa ilikabiliwa na kizungumkuti.

"Mambo yalianza kuwa magumu. Hatukujua tulifaa kuangazia nini. Tuangazie urahisi wa kutumia simu, kudumu kwa betri au ukubwa wa simu?," anasema.

"Ukifikiria kuhusu betri, tulikuwa na simu zingedumu na moto wiki nzima. Kisha, una simu hii mpya yenye nguvu sana ambayo unahitaji kuichaji kila siku. Sasa utaitangaza vipi kwa mteja?"

Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na kampuni ya Microsoft mwaka 2014.



Chanzo:BBC Swahili
 
TECNO ni kama walichukua nafasi ya Nokia,maana wanatengeneza simu za viwango na gharama tofauti.
 
Manager wa Nokia kuna siku alikua anahojiwa na BBC akasema kilichoikuta kampuni ya Nokia ni kua Ulimwengu unakimbia Technology inachange kwa kasi mno ni kama tulilala na kuamka ghafla kukuta mambo yamebadilika na ningumu tena kuenda nayo sawa.
 
TECNO ni kama walichukua nafasi ya Nokia,maana wanatengeneza simu za viwango na gharama tofauti.
 
Uchumi wa unaotegemea biashara ya teknolojia kama simu na computer ni bubble economy, muda wowote mambo yanabadilika na uchumi unakufa kama bubble linavyopasuka
 
TECNO ni kama walichukua nafasi ya Nokia,maana wanatengeneza simu za viwango na gharama tofauti.
mimi hadi leo Tekno naiona kama simu flani mchina mchina hivi, na nikiilinganisha na Nokia, Nokia naona ni ya viwango vya juu sana
 
Binafsi sijawahi kuvutiwa na smartphone za Nokia kabisa.
Ila katika vitochi wao ndio wafalme.
Yeah, mwenyewe hivyo hivyo....NOKIA kwenye smartphone wamefeli, ila za tochi zile dah hakuna wa kuwafikia, ndio maana siikubali Tekno hadi leo
 
TECNO ni kama walichukua nafasi ya Nokia,maana wanatengeneza simu za viwango na gharama tofauti.
 
mimi hadi leo Tekno naiona kama simu flani mchina mchina hivi, na nikiilinganisha na Nokia, Nokia naona ni ya viwango vya juu sana
Mkuu tupo sawa pia katika hili.
TECNO naziona kwa watu tu,hii brand sijawahi na wala sitokaa niitumie.
Bora Huawei.
 
Back
Top Bottom