Kwanza tuanze kwa kuliaddress hili kama jipu. Kiukwel kila halmashauri huwa na utaratibu wake wa kupanda madaraja ingawa vigezo huwa havitofautiani sana. Kwa mfano; mwaka huu vigezo vya jumla vya kupanda madaraja; waajiliwa wote-, waliopandishwa vyeo wote-, waliobadilishiwa muundo wa utumishi wote- 2013 pamoja na wastaafu watakaostaafu kuanzia mwaka ujao wa fedha wanapewa kipaumbele ili kuboost pension zao ambao pia walifikia mwisho wa kupanda madaraja nao wanatakiwa wapande immediate maana serikali ilishafungua madaraja. Sasa njoo halmashauri sound zinaanza
mara kuna viporo vya 2012,
mara nafasi chache tutapandisha wastaafu tu
mara vigezo hamjakidhi mpaka mfikishe miaka 4 toa mwaka mmoja wa kuthibitishwa.
Haya ndio first lady aliahidi atamwambia bwana mkubwa. Kiukwel mishahara yetu ni midogo lakini tusipopandishana kwa wakati mnatufanya tuchukie hata kazi huku kwetu hamnaga posho i.e nyumba, usafiri, ya kikao si chochote, wala marupurupu wala warsha wala makongamano wala hospitality fund sisi ni salarly to salary; mwezi hadi mwezi; mwaka to mwaka mpaka tumetokea mwaka wa tatu. Tafadhari tupandisheni madaraja tumesubiria for 3 good years mbwembwe hatuzihitaji by the way tumeshachoka na sound za halmashauri.