Kuoza kwa vitu(chakula) na kutokea kwa funza

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
3,251
6,790
Kuoza kwa vitu ni badiliko la kikemikali linaloambatana na kuvunjika vunjika kwa maada za kioganiki na kuzalisha kampaundi ndogo ndogo kama vile asidi,gesi na baadhi ya elementi kama kaboni na nitrogeni.

Kuoza kwa vitu ni jambo muhimu linalofanya maisha yaendelee,kwani kuoza husaidia kurusha nutrients ambazo mnyama au mti ulizipata kwa kuzila kabla ya kufa.

Kuoza kwa vitu husababishwa na bacteria na fungi wanaozalisha vimeng'enya vinavyotumika kumeng'enya kiumbe kilichokufa au chakula

Chakula kinapooza uzalisha nutrients mbalimbali.na hata gesi ambazo utumiwa na viumbe wengine kwa ajiri ya ukuaji wao.

CHANZO CHA FUNZA

funza(maggots) kwenye chakula kilichooza ni hatua ya pili ya ukuaji wa inzi(larva stage) kuelekea kwenye inzi kamili.

inzi jike hutaga mayai kwenye vitu vinavyooza kwa ajiri ya urahisi wa kupata chakula na nutrients nyingine kwa ukujaji wa mayai.

mayai yanapokomaa hubadilika na kuingia hatua ya pili ambayo ni funza,watakaobadilika kuwa buu(pupa) na hatimaye inzi kamili
 
Ni vpi kwa mfano chakula kilichopikwa kikapakuliwa kwenye hotpot kikiachwa humo mda fulan ukija kufunua utakuta funza sasa huyo nzi alitaga sa ngapi?
Chakula kikihifadhiwa vizuri ndani ya hotpot kiasi cha kutoruhusu mwingiliano toka nje kamwe hutokuta funza
 
Ni vpi kwa mfano chakula kilichopikwa kikapakuliwa kwenye hotpot kikiachwa humo mda fulan ukija kufunua utakuta funza sasa huyo nzi alitaga sa ngapi?
Chakula ulichokipika,kilichukua mda gani mpaka kuwekwa kwenye hotpot? je hotpot umelitoa kwenye mazingira gani?.

Ikiwa utahakikisha hakuna inzi anayetaga hata kidogo kwenye chakula na kwenye hotpot huwezi kukuta funza,ingawa chakula kitaoza ukikiacha mda mrefu.
 
Chakula kikihifadhiwa vizuri ndani ya hotpot kiasi cha kutoruhusu mwingiliano toka nje kamwe hutokuta funza
Hiyo ni kweli lakini badala yake utakuta aina fulani ya fangasi ambao hufanya kazi sawa na ile ya funza, kuozesha chakula ili ecosystem iendelee. Kwa hiyo baada ya muda utaona chakula kinaoza kama kawaida.
 
sorry hivi kuna tofauti gani kati ya mwanasayansi na mwanafalsafa?
Mwanasayansi anatueleza kivipi? kitu kimetokea,wakati mwanafalsafa anatueleza kwanini? kitu kimetokea.

Nafikiri ni hivyo kiongozi

In other words,Philosophy is all about Metaphysics and conjecture.
 
wakuu leo nimeona tujadili mada tajwa hapo juu je nikwanini vitu vinapooza hutowa funza ,kwa mfano
nguruwe akianza kuoza haitachukua siku zaidi ya tatu unamkuta teyari ameanza kutoa funza je funza hutokea wapi ?
 
Unapokufa Bacteria/Enzyme zinazo digest chakula zinaanza kukutafuna
 
Back
Top Bottom