Kurutu wa Mungu
JF-Expert Member
- Oct 23, 2017
- 366
- 571
Habari za sasa hivi Wana JF,
Bila kupoteza muda niko hapa kuomba USHAURI Juu ya ndoto inayonitesa. Huu ni mwaka wa 4 sasa, iko hivi kuna jamaa tulikua nae na kucheza pamoja toka utotoni huko kijijini kwetu, hata shule ya msingi tulisoma pamoja, tukaachana mwaka 2005 nikiwa darasa la 6 ambapo mimi nilihamia mkoa mwingine
Toka hapo nilikuwa sina mawasiliano naye wala ukaribu wa aina yoyote maana sikurudi tena kijijini hadi mwaka 2015 mwezi wa 8 nilipoenda kwa dharura ya msiba wa mjomba kwa vile nilienda kwa dharura nilikaa siku moja asubuhi nikaondoka kurudi ninapoishi, na huyo jamaa nilionana nae nikiwa naelekea kupanda gari kurudi.
Kwa vile alikuwa rafiki yangu mkubwa utotoni alinisihi nisiondoke siku hiyo alinitaka nilale niondoke asubuhi yake tuongee na kukumbushana story zetu za utotoni hadi akawa ananiahidi kuna jogoo nyumbani kwao nikikubali kulala atanichinjia na atanitafutia zawadi ya samaki nirudi nao mjini, maana Kijiji kiko kandokando ya ziwa Victoria
ilimkatalia maana nilikuwa nimepewa ruhusa ya siku 5 kazini na kutoka ninapoishi hadi kufika huko nilikua nimeshapoteza siku 2. Tulipeana tu namba za simu nikaondoka baada ya hapo niliwasiliana nae kama mara 3. Ilipofika mwaka 2016 mwezi wa7 nilipata taarifa kuwa huyo jamaa amefariki kwa kuanguka juu ya mti wa mwembe. Kwa vile nilimfahamu nilisikitika sana, cha kushangaza toka huo mwaka wa 2016 nimekuwa nikimuota mara kwa mara yaani haupiti mwezi bila kumuota
Mwanzoni nilijua hali hiyo ingepotea lkn imekuwa sivyo, nilijaribu kuwashirikisha ndugu wa karibu wakaniambia niwe ninasali, nimejaribu kufanya hivyo lkn bado nimekuwa naota tuko pamoja tunaongea. Mwaka Jana mwezi wa 9 nilienda kusalimia kijijini nikafika hadi kwao kuwapa pole na kuona kaburi lake pia nilijaribu kuuliza juu ya kumuota mara kwa mara. Wanakijijini nilioongea nao wakaniambia kifo chake kimejaa utata na kuna mauzauza mengi yanawatokea toka siku ya msiba wanadai alikuwa anawagongea milango usiku na kujitambulisha kuwa ni yeye kama wamebakisha chakula wampe ale ana njaa
Mara ya mwisho kuota nijuzi nimeota niko nae namuuliza "" kwanini tuko pamoja wakati wewe ulishakufa?"" yeye alianza kulia sasa Kuna sauti ikawa inanijibu lkn simuoni huyo anayeninibu ""Huyu hajafariki na usiwe unamuuliza hilo swali anajisikia vibaya"" ghafla upepo ukavuma halafu wakashuka watu wa3 kumchukua na mimi wakanishika tukaanza kupaa yaani tunaenda kwa spidi kali tukawa tunaelekea ziwani nikawa naona mazingira ya kijijini napita juu ya mapaa ya nyumba za nyasi nikawa napiga kelele ghafla, nikashituka nikawa natoka jasho na moyo unaenda mbio
Kiukweli nikitoka usingizini huwa nakosa amani na inanichukua mda kupata tena usingizi, Je ni nini kinafanya niwe namuota?
Na suluhisho ni nini?