Kuopoa mrembo mtandaoni.....ha ha ha..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuopoa mrembo mtandaoni.....ha ha ha.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Boss, May 30, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  Mume aumbuka, ampa 'kichapo' mkewe  MWANAUME mkware nchini Uturuki ameumbuka baada ya kugundua kuwa mwanamke aliyemfungia safari kwenda kumuona face to face baada ya kutongozana kwa kutumia ujumbe wa simu kwa muda mrefu alikuwa ni mkewe aliyekuwa akimchunguza kama ana kimada nje.

  Mke wa mwanaume huyo mkazi wa mji wa Trabzon, alikuwa akimshuku mumewe kuwa na kimada nje kutokana na mabadiliko ya tabia zake aliyoyaona.

  Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina moja la Hulya(22) alisuka mpango wa kupima uaminifu wa mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Murat.

  Hulya ili kujua kama mumewe ana kimada nje aliamua kuchukua simu ya ndugu yake na kuanza kumtumia mumewe meseji za kimapenzi akijifanya kuwa yeye ni mwanamke aliyevutiwa naye na alihitaji wawe na uhusiano wa kimapenzi.

  Mumewe imani ilimshinda, alinasa kwenye mtego huo na kuanza kujibu meseji hizo kwa SMS kibao za mapenzi mpaka kufikia kupanga siku na sehemu ya kukutana ili waanze kujivinjari.

  Mume huyo bila kujua kuwa mwanamke aliyekuwa akitumiana naye meseji alikuwa ni mkewe, alimuaga mkewe kuwa anatoka kidogo usiku kuonana na rafiki yake na atachelewa kurudi.


  Huku akiwa na shauku kubwa ya kumuona mwanamke aliyekuwa akitongozana naye kwa simu, mume huyo mkware alipigwa na butwaa baada ya kuona mwanamke aliyejitokeza alikuwa ni mkewe tofauti na hesabu zake alizokuwa akipiga.

  Kwa hasira mume huyo alimshushia kipigo mkewe hapo hapo na kusababisha polisi waliokuwa wakipita karibu na eneo la tukio kuingilia kati na kumkamata.

  Hulya hakuwa na nia ya kumfungulia mashitaka mumewe pamoja na kwamba alimjeruhi lakini polisi waliomkamata Murat waliamua kumshitaki.
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Oyee! Oyee! Wa gwaaan! Dis univesal bwana si mchezo na love ndo starring wa mambo yote na ndivyo maisha yalivyo. Kip on chat online. Yeeah big boss!
   
 3. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Lakini na huyo mwanaume ni ***** kweli, inawezekanaje akasindwa kugundua hata writting za mke wake? kwa ninavyojua mimi writting au muunganikano wa sentensi za sms kuto kwa my wife lazima nijue au nigundue kitu flani then mimi ndo nigeandaa mtego. Huyo mwanaume ni ***** tu.
   
 4. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi soo la jirani linazungumzika kirahisi, omba mungu!!
   
 5. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Si kama so la jirani linazungumzika kirahisi...kusema kweli mke wako kama anakuandikia message lazima utajua tu
  labda kama huyo jamaa kama amekuwa na mawasiliano na huyo mwanamke kwa muda mdogo sana ila kama ni wiki
  na kuendelea yaani ni ngumu sana kwa mwanamke kufanya hivyo na wewe usigundue...this is from my own xp...hehehe!
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Huyo jamaa ni kilaza tu; anashindwa kuelewa lugha ya mtu wake wa karibu! na anarukia mtoni mzima mzima na hajawai kuoga hapo!! bila kupima kina cha maji kwanza!

  karaga baho
   
 7. Causin

  Causin Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman,Iyangalo hy avatar yako imenifurahisha sn,afu imenikumbusha mbali saaaaana.
   
Loading...