Nimepata habari ya kwamba kuna michepuo mipya kama tano imeongezwa, mtoa habari amekumbuka mbili nazo ni; PGE (Physics, Geograpraphy na Economics), CBM (Chemistry, Biology na Math.).....
Miongoni mwa shule zilizopendekezwa ni Galanosi, Ifunda Girls, Pugu, Tosamaganga n.k.
Michepuo iliyopoongezwa ni ya sayansi.
Nikipata michepuo yote na shule nitaongeza, pia kama unazo naomba uongeze.
Asante kwa taarifa hii Kimbori. Inatia moyo kuona kuwa hatimaye Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wameliafiki wazo la kuongeza Combinations mpya hasa zilizo na Masomo ya Fizikia, Uchumi, Hisabati, Kemia na Biolojia. Natumaini EPM na ECM nazo zitakuwemo bila kusahau EBM na PBM.