Wanajamii,
Nimewasalimu.
Nimeanzisha Mada hii tuitafakari na tujaribu kuijadili kwa kina.
Katika mfumo wa Legislature mapema tu baada ya Uhuru, pamoja na Sheria zingine za nchi, Rais alikuwa na uwezo kisheria kumkamata na kumweka ndani mtu yeyote bila kufikishwa mahakamani endapo Angeridhika mtu huyu ni hatari kitabia, kiusalama au vyovyote vile na kwamba alikuwa hafai kuishi na jamii.
Sheria hii ilimpa nguvu Rais kudhibiti makosa ya Ufisadi, ubadhirifu wakati mwingine ulanguzi wa madawa ya kulevya hata pombe haramu!
Sababu baada ya Tume ya Rais wakati ule ingekubaini kuwa wewe ni miongoni katika washiriki wa matendo hayo na kukufikisha mezani kwa Baba wa Taifa ulikuwa umekwisha!
Mzee Ruksa alipoingia madarakani baada ya kusumbuliwa na tume za haki za binadamu ikabidi aiondoe sheria hii. Hapa Ndipo mapapa wa Bahari walipopata mwanya wa kutamba na kupora pesa za wavuja jasho sababu mahakama ndio ilipitishwa kuwa chombo muafaka kutatua maswala ya ubadhirifu, rushwa, mihadarati n.k. kitu ambacho hakikuwatisha wengi sababu wengi wao walikuwa na uwezo au mbinu ya kupenya.
Kwa nini sheria hii isirudishwe tukapata amani na usalama wa Mali za umma na rasilimali za nchi?