Kuondoa michango ya wananchi mashuleni ni sahihi?

KARUNGU YEYE

New Member
Dec 21, 2015
2
0
Wadau napata wakati mgumu saaaana pale napoliangalia hili swala la serikari yetu tukufu kugharamia gharama za elimu kwa nchii nzima hususani katika sekta ya miundombinu!!!

Naamini katika mikoa yetu ya tanzania miundombinu ya shule zetu haifanani hata kidogo.Mfano ukianza na mkoa wa Kilimanjaro.Hakika na amini madarasa yaliyojengwa katika shule za mkoa huu wingi wake hauwezi lingana na madarasa yanayopatikana mikoa kama Kagera, na Kigoma.

Uhitaji wa miundombinu kwa mikoa kama simiyu,shinyanga,mara,na mikoa mingine mingi haiwezi linganishwa na mikoa kama Mwanza,Dar,Kilimanjaro nk...

Je, serikali itapeleka pesa hizi za miundombinu kulingana na uhitaji wa wilaya au zitagawiwa kwa usawa?

Kwa namna ya pekee bila kupepesa macho naamini ujenzi wa darasa moja unaweza gharimu zaidi ya mill 30 za kitanzania kama shule za msingi tu kwa nchii zipo 17,000.

Tuseme katika shule hizi zaidi ya shule 710,000 zina upungufu wa madarasa na madawati.Je, gharama hizi zitawezekana?

Naipongeza serikali yetu kwa nia ya dhati ya kutaka kutoa elimu bureeee ila naamini bado tunahitaji kufikiri kwa kina na kuendesha elimu kulingana na mazingira pamoja na mahitaji ya eneo husika.
 
Naomba niunge mkono hoja.

Pia, kuna shule ambazo wazazi (kamati za shule) wamejitahidi sana kutafuta wahisani na kuchangisha wazazi wakaweza kuboreshahadhi ya shule kuwa kama binafsi. Shule hizi zina maji na umeme (bili za maji na umeme zinalipwa kwa michango ya wazazi), Computers, printers, photocopier (Walinzi, stationery), watoto wanakula mchana na yote haya ni kwa michango ya hiari ya wazazi. Mitihani yao ya kila wiki inakuwa printed. Vyoo vimejengwa vya kisasa na vinahudumiwa na wafanyakazi vibarua. Gharama za vibarua, wapishi, madawa ya vyooni ni michango ya wazazi.

Swali langu ni kama serikali itagharimia haya yote au la. Baada ya serikali kutangaza michango kusitishwa, hizi shule zimezidiwa na watoto wanaopelekwa kuandikishwa kwani zina ubora wa pekee. Shule kama hizi zitafanyaje?
 
Hiki kizazi cha dotcom kuna jambo ambalo hamlielewi.Kuchangia elimu ni mikakati ya kifisadi.Kabla ufisadi haujaingia katika kiwango tulichonacho sasa mzazi kazi yake ilikuwa ni kununua uniform tu.Vitu vingine vyote mtoto alikuwa anapata shuleni.Mimi nilisoma enzi hizo na ni shuhuda.Kama iliwezekana enzi hizo inawezekana hata zaidi leo.Acheni serikali itimize wajibu wake kwa watu wake kwa kuwa nia ipo na uwezo upo.Huyu ni Rais anayependa watu wake sana.Huu ni mwanzo tu

Kujibu swali lako ni kwamba kuondoa michango mashuleni ni sahihi kabisa.

Wengi wetu hili suala mnalichukulia juu juu bila kutafaksri kwa kina juu ya uwezo wa serikali kiuchumi. Hebu waseme juu ya wazazi kuchangia remedial na Mitihani ya week. Kwa mazingira ya mjini kumrudisha mtoto SAA name in kumtafutia majanga kwani atakuwa mzururaji kwa kukosa waangalizi ambao wengi wa wazazi huwa kwenye pilika za maisha. Tafiti zipo wazi tafuteni mzisome. Wazazi waachwe wawe guru juu ya michango ya taaluma, majengo na mambo mengine bila kuwekewa mipaka kwani yote hayatawezekana kwa mwaka mmoja.
 
Hiki kizazi cha dotcom kuna jambo ambalo hamlielewi.Kuchangia elimu ni mikakati ya kifisadi.Kabla ufisadi haujaingia katika kiwango tulichonacho sasa mzazi kazi yake ilikuwa ni kununua uniform tu.Vitu vingine vyote mtoto alikuwa anapata shuleni.Mimi nilisoma enzi hizo na ni shuhuda.Kama iliwezekana enzi hizo inawezekana hata zaidi leo.Acheni serikali itimize wajibu wake kwa watu wake kwa kuwa nia ipo na uwezo upo.Huyu ni Rais anayependa watu wake sana.Huu ni mwanzo tu

Kujibu swali lako ni kwamba kuondoa michango mashuleni ni sahihi kabisa.

Ninasikitika kuwa na wewe ulisoma wakati ule. Inawezekana na wewe una mawazo mgando ama uliingia darasani hukuuona ubao. Kama uliuona, maandishi yalikupa shida, kama uliona maandishi, basi hukuyaelewa, kama uliyaelewa, huwezi kuyachambua yakaweza kukupambanulia kuwa muda una nafasi yake kwenye mzunguko wa dunia.

Miaka 30 ya "neglect" imesababisha shule zikatofautiana. Sio shule zote zinahitaji madawati, pia sio zote zinahitaji majengo. Wale waliotambua kuwa serikali haichangii kwenye shule walianza kujiwajibisha wenyewe ili watoto wao wasikose vyoo, wasishinde na njaa shuleni nk hivyo wakaamua kuchangia, kwa hiari au shuruti. Shule hizi zimeendelea kuwa na viwango tofauti na zingine. Kuzirudisha miaka 30 nyuma ili zifanane na zile za wengine itakuwa ni makosa makubwa.

Wakati wewe na mimi tunasoma, tofauti kati ya shule na shule zilikuwa ndogo sana, ukiachia shule kama Kibaha (ambazo zilikuwa kama college ya University). Huwezi ukazifananisha zote leo kwa amri moja. Ninachotaka kushauri ni kuwa hii amri ya kufuta michango pia iangalie mahitaji ya shule husika ili kwamba kama serikali haitamudu kutimiza mahitaji yote ya shule kutegemeana na gharama halisi, waruhusu kamati za shule kushawishi wazazi waliokuwa wanalipia huduma kwa ajili ya watoto wao waendelee kufanya hivyo. Tusiwe kama tunarudisha watoto wote chekechea kwa sababu tumebadilisha mtaala wa masomo. This is a simple logic, ukishindwa kuelewa tusibishane, tuishie hapa.
 
Wadau napata wakati mgumu saaaana pale napoliangalia hili swala la serikari yetu tukufu kugharamia gharama za elimu kwa nchii nzima hususani katika sekta ya miundombinu!!!

Naamini katika mikoa yetu ya tanzania miundombinu ya shule zetu haifanani hata kidogo.Mfano ukianza na mkoa wa Kilimanjaro.Hakika na amini madarasa yaliyojengwa katika shule za mkoa huu wingi wake hauwezi lingana na madarasa yanayopatikana mikoa kama Kagera, na Kigoma.

Uhitaji wa miundombinu kwa mikoa kama simiyu,shinyanga,mara,na mikoa mingine mingi haiwezi linganishwa na mikoa kama Mwanza,Dar,Kilimanjaro nk...

Je, serikali itapeleka pesa hizi za miundombinu kulingana na uhitaji wa wilaya au zitagawiwa kwa usawa?

Kwa namna ya pekee bila kupepesa macho naamini ujenzi wa darasa moja unaweza gharimu zaidi ya mill 30 za kitanzania kama shule za msingi tu kwa nchii zipo 17,000.

Tuseme katika shule hizi zaidi ya shule 710,000 zina upungufu wa madarasa na madawati.Je, gharama hizi zitawezekana?

Naipongeza serikali yetu kwa nia ya dhati ya kutaka kutoa elimu bureeee ila naamini bado tunahitaji kufikiri kwa kina na kuendesha elimu kulingana na mazingira pamoja na mahitaji ya eneo husika.

Mtazamo wako ni mzuri ila ninachofahamu ni kwamba fedha itakayopelekwa direct Shuleni ni ya recurrent (fedha ya uendeshaji),kwa fedha ya miradi (development) kama ujenzi ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine ya shule itaendelea kupitia Halmashauri kulingana na bajeti iliyopitishwa
 
Hiki kizazi cha dotcom kuna jambo ambalo hamlielewi.Kuchangia elimu ni mikakati ya kifisadi.Kabla ufisadi haujaingia katika kiwango tulichonacho sasa mzazi kazi yake ilikuwa ni kununua uniform tu.Vitu vingine vyote mtoto alikuwa anapata shuleni.Mimi nilisoma enzi hizo na ni shuhuda.Kama iliwezekana enzi hizo inawezekana hata zaidi leo.Acheni serikali itimize wajibu wake kwa watu wake kwa kuwa nia ipo na uwezo upo.Huyu ni Rais anayependa watu wake sana.Huu ni mwanzo tu

Kujibu swali lako ni kwamba kuondoa michango mashuleni ni sahihi kabisa.

jibu zuri sana hili nimelipenda.
 
Back
Top Bottom