Kuombwa msaada ya kifedha na watu wengi

Kuombwa msaada ya kifedha na watu wengi

kiongozi afadhali wewe wanaokuomba wanakujua,mimi huko mitaani unakuta jitu hata akikujuhi linakuomba 1000 yaani mi kesi za namna hii ndio nyingi mpaka nachukia,halafu afadhali wangekuwa watoto ni mijitu mizima kabisa,
Bro mi nilihamia nyuma hata mweZi Sina mpangaji mwenzangu anakuja nikopa laki 3 hanijui simjui zaidi ya salamu.
 
Sionww tu mkuu. Hili ni janga. Ratio ya dependants inatofautiana mtu na mtu , 1:4, 1:8, 1:10, 1:20, mwingne 1:50 hadi 1:500 n.k

Kama kipato chako ni kidogo na una dependants wengi kuendelea ni ngumu mnooo. Roho ngumu yatakiwa.

Kuna uzi humu ndani wa msukuma ana tegemezi kibao mpaka mke wake anamuona mtu alierogwa. Mshahara 1m+ lkn ana maisha kama ya mwalimu wa Namtumbo.
 
Nikiri kwanza sipo Vizuri sana kwenye roho ya kikauzu.

Ndugu:Nikope laki tatu nimalizie Kodi.

Ndugu:Nimekwama mwanangu(sio mama mzazi) Sina kitu nichangie chochote.

Rafiki:Naomba elfu kumi nisogeze siku pesa yangu bado haijatoka.

Ndugu:Nina mpango wa kufungua biashara nitakucheki basi uniongezee mtaji usiache pokea simu yangu.

Rafiki:Nikope elfu 20000

Ndugu:Nikope laki 200,000 nitakupa.

Rafiki:Nikope elfu 20,000 nimekwama.

Rafiki:Nimekwama Kaka nicheki la ten.

Mpenzi:Simu yangu mbovu na mpango wa kununua nyingine pesa ya haijakamilika.

Ndani ya tarehe 4/6/2019 Hadi leo hii 9/6/2019.Nimepokea request hizo hapo juu za pesa,kiukweli napitia kipindi kizito sana cha kujifunza kusema Hapana maana sikuzaliwa na roho ya kusema Hapana watu wangu wa karibu wanapokuwa na shidA ila hii inaniwia vigumu Sana.

Hivi kwenye ulimwengu wa kiroho hii ina maana gani?Kuna mtu anakutana na situation kama hii kwenye maisha yake?

Mnaweza kupambana na hali hii??Nimekataa request nyingine sana hapo juu nyingine Ni za watu karibu Sana.

Mwezi uliopita nimekopa watu jumla ya laki 2 tena kwa kubalance mambo kweli kweli.

Note:Sina maisha magumu ila sio tajiri kiasi cha kuwa na uwezo wa kusaidia watu kiwango hicho hapo.
Situation yangu yafanana na yako napata shida sana kutomsaidia mtu akiomba. Na hii ime/inanigharimu sana. Sasa niko kwenye kipindi cha kufanya mageuzi. Ushauri wangu,
1. Wanaokuja kuomba (sio kukopa) wape kama una uwezo wa kuwapa bila kukuathiri kiuchumi (kama iko ndani ya uwezo).
2. Achana na kukopesha watu labda kama ni ndugu wa karibu sana, na pia kama uwezo unaruhusu na shida yake ni genuine. Uzoefu wangu ni kwamba hapa kwenye kukopa ndio kwenye tabu. Watu wenye uaminifu wa kurudisha kwa wakati bila kusukumwa wala kugombana kwanza ni kama hawapo. Matokeo yake ni kupata makwazo nafsini.
 
Mkuu heshima kwako, ushauri wangu kwako :
1. Saidia kwa kadiri ya uwezo wako bila kuathiri mipango yako
2. Weka vipaumbele mfano kuchangia wagonjwa, mahitaji ya msingi ya shule nk badala ya kuchangia harusi au kitchen party
3. Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya pesa utakazowapa ndugu na marafiki hazitarudi, hii ni mojawapo ya sababu kuu inayoharibu undugu na urafiki hivyo kama ukiamua kusaidia toa kiasi ambacho hata usiporudishiwa hakitaathiri uhusiano wenu
4. Toa msaada kwa sababu ya utu na usitegemee na wewe kusaidiwa siku ukiwa na uhitaji, binadamu hubadilika haswa wanapofanikiwa
 
Asante sana kaka,nitafanyia kazi Hilo hapa toka nimeanza kazi Kuna kama milion 5 hivi zipo kwa watu na hamna mpango wa kuzipata
 
Mkuu heshima kwako, ushauri wangu kwako :
1. Saidia kwa kadiri ya uwezo wako bila kuathiri mipango yako
2. Weka vipaumbele mfano kuchangia wagonjwa, mahitaji ya msingi ya shule nk badala ya kuchangia harusi au kitchen party
3. Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya pesa utakazowapa ndugu na marafiki hazitarudi, hii ni mojawapo ya sababu kuu inayoharibu undugu na urafiki hivyo kama ukiamua kusaidia toa kiasi ambacho hata usiporudishiwa hakitaathiri uhusiano wenu
4. Toa msaada kwa sababu ya utu na usitegemee na wewe kusaidiwa siku ukiwa na uhitaji, binadamu hubadilika haswa wanapofanikiwa
Kweli kabisa Kaka, Asante
 
Shukuru Mungu amekuweka kwenye position ya kupokea maombi. Sidhani kama ungependa kuwa kwenye position ya kuomba.
Umeongea maneno mazito ila situation kama hii hunikuta hata mimi na huwa najiuliza majukumu yote haya niliyonayo bado kuna watu wananiona kuwa ni wa msaada kwao hvyo huwa naomba rehema za Mungu zinishukie niwe na uwezo wa kusaidia wahitaji #second class citizen
 
Nikiri kwanza sipo Vizuri sana kwenye roho ya kikauzu.

Ndugu:Nikope laki tatu nimalizie Kodi.

Ndugu:Nimekwama mwanangu(sio mama mzazi) Sina kitu nichangie chochote.

Rafiki:Naomba elfu kumi nisogeze siku pesa yangu bado haijatoka.

Ndugu:Nina mpango wa kufungua biashara nitakucheki basi uniongezee mtaji usiache pokea simu yangu.

Rafiki:Nikope elfu 20000

Ndugu:Nikope laki 200,000 nitakupa.

Rafiki:Nikope elfu 20,000 nimekwama.

Rafiki:Nimekwama Kaka nicheki la ten.

Mpenzi:Simu yangu mbovu na mpango wa kununua nyingine pesa ya haijakamilika.

Ndani ya tarehe 4/6/2019 Hadi leo hii 9/6/2019.Nimepokea request hizo hapo juu za pesa,kiukweli napitia kipindi kizito sana cha kujifunza kusema Hapana maana sikuzaliwa na roho ya kusema Hapana watu wangu wa karibu wanapokuwa na shidA ila hii inaniwia vigumu Sana.

Hivi kwenye ulimwengu wa kiroho hii ina maana gani?Kuna mtu anakutana na situation kama hii kwenye maisha yake?

Mnaweza kupambana na hali hii??Nimekataa request nyingine sana hapo juu nyingine Ni za watu karibu Sana.

Mwezi uliopita nimekopa watu jumla ya laki 2 tena kwa kubalance mambo kweli kweli.

Note:Sina maisha magumu ila sio tajiri kiasi cha kuwa na uwezo wa kusaidia watu kiwango hicho hapo.
Bro nisaidie namb yako
 
Kuna ndugu hawapendi kujishuhulisha kazi kuomba omba nimeshawafungia vioo mwaka huu,kuna rafiki nae aibu haoni ana kazi nzuri serikaln kazi kuniomba omba pesa kila mara na sijawah kumpa na urafiki umekufa .

Kila mtu anapaswa kufanya mambo kulingana na kipato chake,kwakua kila mtu anamajukumu yake kuombana hela ni kubebeshana majukumu yasio ya lazima.

kuomba omba hela huanza na watu wanaofanya mambo ingali kipato chao hakiruhusu kama kupanga nyumba ya bei gali kuliko kipato,kupeleka mtoto shule ya bei ghali,magari wasiyoweza kuyahudumia,starehe kupitiliza n.k
 
Angalia ambao unaona unaweza kuwasaidia kwa sasa wengine unawaambia wakucheck kipindi kingine..

Na Kama mtu anataka hela nyingi ambayo huna na unatamani uupe basi unampa uliyonayo Kama nusu ya pesa mfano kaomba 200,000 we unamwambia unaweza kumsaidia 100,000.
Wale wa muhimu wasaidie.
Wasio wa muhimu wapotezee, na ikiwezekana kikauzu.
SINA.

Wiki ijayo na wewe watumie meseji kuwaomba msaada wa kifeza.
 
We bado hujakosa ndo maana huwezi kukataa endelea kusaidia ukikosa utawaambia kuwa huna
 
Back
Top Bottom