Lbda uhamie ughaibuni kwa mila za kiafrica hilo swala ni gumu kama wote mnazaa.
Kuna nchi nyingi Ulaya magharibi unakuta watu ni careeer tu hivyo hawana muda wa watoto so hawazai, lakini uzeeni wanajuta na kufa kama anonymous huku serikali ikitaifisha mali zao, ya nini yote hayo?? zaa bwana.
Hii ndio haswaaaa ninachotaka kusisitiza mimi. Na kwa kuongezea, ndugu Leornado hebu tafakari kama na wazazi wetu nao wangesema wanapanga wasizae, tungekuwa wapi sasa hivi???
Yapaswa tusijiangalie sisi tu pekee, lazima tu-focus na mbeleni na hatima ya vizazi vijavyo. Sisi ndio tuna jukumu la kujenga vizazi vijavyo na hatupaswi kulikwepa. Hatupaswi kuwa kianzio cha kuzuia vizazi vijavyo
Uwezekano upo...tatizo ni watu wa nje watachukuliaje uamuzi huo!
Ndugu watu wanafikra tofauti..., kila mtu ana mtizamo tofauti na maisha..., Sio watu wote wenye uamuzi wa kutokuwa na familia.., infact ni percent ndogo sana..., main point ni kwamba kwanini jamii ishinikize kila mtu ajaze dunia?, kupata watoto sio obligation, na inabidi hii issue ifikiliwe na wanandoa kama wapo ready kutunza familia..., sababu kuzaa sio kazi even animals can do that..., lakini malezi its all that matters..., sasa unaposhinikiza watu wazae wakati hawataki ndipo tunapopata malezi mabovu..., I repeat this should be the decision of partners and nobody else.
Leo unaiita percent ndogo, baada ya miaka kadhaa mbele unadhani itabaki hivyo hivyo??!!
Think . . .
CPU.. sasa kama mmoja wao baada ya ndoa ikagundulika au ikatokea sababu ya kutokuweza kuzaa ina maana yule mwingine ana haki ya kuzaa nje ya ndoa au ndoa ivunjike hata kama bado wanapendana?
Hivi haya maneno ya nje kwani ni lazima kuyasikiliza? Huo muda wa kukaa unawasikiliza unatoka wapi? Mimi ni mmoja wa hao ninayepanga kufuata nyayo za hawa wawili!Inawezekana pia kama mtakua mmeoana na kila mmoja ana watoto. Kuna dada aliolewa na mume ambaye ana watoto 3 na yeye mmoja, walichokubaliana ni kutokuzaa mtoto kwa vile wanao tayari. Pia mnaweza kuamua kuishi bila kupata watoto, ila kwa mila zetu za huku inakuwa tabu kweli. Maneno hayatakosekana hapo lawama ni kwa mwanamke hazai.
Hivi since the beggining of mankind umeona population percentage is it declining or increasing...?
watu wasiopenda familia sio wengi because majority ya dada zetu wanapenda watoto, wanapenda familia (human nature) deep down they are mothers...,therefore this percentage will remain to be small.., its a minority..., and that minority haitakiwi ifanye kitu through pressure from the outside na inabidi jamii iwaache na decision yao na sio kuwashinikiza. If its only the case ya kuijaza dunia how many homeless children are there..., Lets start taking care of them first kuliko kusema kwamba kila mtu ana jukumu la kuijaza dunia.
Naona umeanza kunielewa ila bado kuna kitu ambacho huamini kama kitaweza kutokea. Population haiongezeki automatically. Kumbuka HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA.
Hao wanaozaliwa na dada zetu hawawezi kuchange mind wakaishi bila kuzaa wakiona kuna watu wameishi bila kuzaa??
Mi siwezi kukusukuma lazima uzae, ila fahamu future world will be affected by our decisions
Mkuu population growth is exponential na inakuwa kwa kasi sana..., hata ndio maana China kuna limit ya watu kuwa na watoto..., now unless litokee Gonjwa kubwa la kuumaliza ulimwengu au any massive catastrophe then population itaendelea kuongezeka mpaka pale automatically tutakapoanza kufight for resources ndio itaanza kujilimit na itapunguza kasi... Pia kuna incentives mfano Russia nadhani kuna wanaume wachache au vice versa kwahiyo government inatoa incentives kwa watu kuzaa.
Now you cant fight with Human Nature, majority kina dada wanapenda watoto..., that is nature.., ndio maana hata mtoto mdogo wa kike anakuwa anapenda madolls acheze nayo..., kwahiyo mkuu usihofu hii issue ni ya wachache lakini tusiwape shinikizo kwamba they have a duty to perform ya kujaza ulimwengu...
Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?