Habari mkuu,
Sio kukupinga, ila kwa kawaida (kwa sheria za eBay) wauzaji wengi sana wanatumia mfumo wa kulipia wa PayPal.
Na wengi unakuta wanaweka wazi kabisa "ONLY PAYPAL ACCEPTED"
Wa kulipia na Kadi bado wapo, ila kwa wengi wao hawatahitaji PIN yako (wanaofanya hivyo ni wezi). Watakachohitaji sana sana ni card number, expiration date, na CVC bas. Ambazo hizi zinatumika kuhakikisha uhalisia (authenticity) wa kadi yako. Wewe mwisho wa siku ndio una'authorize pesa itoke kwenye account kwenda kwa muuzaji.
Halafu, mkuu kuwa makini na kununua bidhaa kisa umeona bei iko chini.
Jaribu hata kuangalia ITEM DESCRIPTION upate kujua kama bidhaa ni mpya/used/sold for parts. Items zingine unakuta bado ziko kwenye listings lakini seller hayuko behind that anymore, au seller yuko kiwasiwasi (shady).
Angalia pia "Approval Ratings" za huyo muuzaji. Mara nyingi binafsi nimejiwekea imani na Seller mwenye ratings kwanzia 96%
View attachment 629268
Angalia hapo utaona Seller wa bidhaa hii ana approval ratings ya kuaminika kabisa 100%.
View attachment 629272
Then click hapo, utaona ratings from Positive, Neutral to Negative ndani ya Mwezi mpaka Miezi 6 iliyopita.
Sasa angalia Neutral na Negative comments, angalia kama kuna hata moja inahusiana na "Item Number" ya bidhaa unayotaka kuinunua.
Pia jinsi unavyoona malalamiko mengi changanya na akili zako ufanye maamuzi ya busara kabla hujaamua kununua toka kwa huyo muuzaji.
View attachment 629273
Hii ndio item namba ya bidhaa. Angalia hii then cheki kwenye reviews kama item number yako (ambayo ndio bidhaa) imetajwa kokote (iwe kwenye positive, neutral, au negative reviews).
View attachment 629274
Angalia reviews za wanunuzi waliowahi nunua toka kwa muuzaji huyo. Wanaongeleaje huduma/bidhaa zake.
Zaidi ya hayo, WASILIANA na muuzaji. Na soma vizuri Item Description, usije agiza parts/scrap au used items kisa kufurahia bei che.
Yangu ni hayo tu.