Kunuka mdomo kumesababisha niachwe na mpenzi, tafadhali nisaidieni

Hahahaaa katika vitu vigumu kuvumilia ktk mapenzi mojawapo ni hilo kunuka mdomo, soksi, kwapa la beberu duu mimi siwezi kabisa
nilitolewa out na mkaka mzur ila alkua na hlo tatizo kila muda anataka aongee nilikua mpole kwel had nikasifiwa,ilinibid niwah kuondoka kisingizio cha kuwa na emergency kumbe uvumilivu ulinishnda
 
Habari wana jamvi,

Huyu mwanamke toka nimempata hataki nimpige kiss, denda na hata tukiongea huwa anaziba pua.

Sasa jana tumekosana ndo kanambia domo langu linatoa harufu kama choo, nikaishwa mpaka pozi.

Nikakumbuka matukio yote nikiwa na wadau nikiongea tu wanaziba pua.

Dah huu mdomo huu mbona naupiga mswaki kila siku au nilikula mavi kipindi niko mtoto?
Dah! Hata medi oral nzuri inakata harufu ya domo
 
Habari wana jamvi,

Huyu mwanamke toka nimempata hataki nimpige kiss, denda na hata tukiongea huwa anaziba pua.

Sasa jana tumekosana ndo kanambia domo langu linatoa harufu kama choo, nikaishwa mpaka pozi.

Nikakumbuka matukio yote nikiwa na wadau nikiongea tu wanaziba pua.

Dah huu mdomo huu mbona naupiga mswaki kila siku au nilikula mavi kipindi niko mtoto?
Yanayosababisha mdomo kutoa harufu mbaya

Yanayosababisha mdomo kutoa harufu mbaya.jpg

Kwa ufupi

Kwa kawaida mdomo na pua hutoa pumzi nje ambayo huwa na harufu asilia ambayo haiwezi kumkera mtu mwingine, lakini mara nyingine hali hiyo inaweza kujitokeza kwa mtu kutoa pumzi yenye harufu mbaya.

By Dk Shita Samwel, Mwananchi
Katika maisha ya kila siku inawezekana umewahi kukutana na mtu ambaye ukiwa karibu naye kimazungumzo, utagundua anatoa harufu mbaya mdomoni.

Kwa kawaida mdomo na pua hutoa pumzi nje ambayo huwa na harufu asilia ambayo haiwezi kumkera mtu mwingine, lakini mara nyingine hali hiyo inaweza kujitokeza kwa mtu kutoa pumzi yenye harufu mbaya.

Pengine watu wa karibu au wanaokutana na mwathirika wa hali hii, wanaweza wakadhani mtu huyo ni mchafu mwenye na tabia ya kutopiga mswaki au kutosafisha kinywa chake vizuri.

Wengi hawajui kuwa mtu huyo anaweza kuwa na tatizo linalojulikana kitabibu kwa jina la halitosis, ambalo maana yake ni kutoa pumzi ama mdomoni au puani.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kukumbana na kunyanyapaliwa na wanajamii wanaomzunguka kiasi cha kuweza kumsababishia matatizo ya kisaikolojia.

Mwathirika anaweza kupata na tatizo la hofu iliyopitiliza anapokuwa katika jamii; anaweza akajinyofoa kutoka katika jamii na kujitenga na baadaye anaweza kupata sonona.

Ugonjwa wa halitosis
Karibu asilimia 20 ya watu duniani wanakumbwa na ugonjwa huu na hivyo kukimbilia kwa wataalamu wa afya ya kinywa.

Hufika kwa wataalamu hawa wakidhani wana magonjwa ya kinywa ikiwamo mashimo katika meno, kulika kwa meno, kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi.

Ukweli ni kuwa si wagonjwa wote wenye kutoa pumzi yenye harufu mbaya wana tatizo halisi la halitosis, kati ya asilimia tano hadi 72 wanaofika katika huduma za afya hugundulika kuwa hawana tatizo hili moja kwa moja.

Tatizo la kutoa pumzi yenye harufu mbaya ambalo ndiyo ugonjwa halisi, linasababishwa na uwapo wa mrundikano wa bakteria katika uvungu wa fizi na nyuma ya ulimi karibu na koo.

Kinywa kwa ujumla, kikijumuisha meno, fizi, ulimi na vifuko vya mate kinaweza kuwa ni maficho mazuri kwa mamia ya bakteria. Ndiyo maana inaaminika tatizo la harufu mbaya mdomoni ni kinywa chenyewe.

Kinywani pekee kuna karibu jamii 600 za bakteria ambao huambatana na mabaki ya vyakula tunayokula kila siku. Kuwapo kwa protini ya kwenye mate na protini ya vyakula tunavyokula na uvunjwaji wa mabaki yake na bakteria waliopo mdomoni, ni chanzo cha kuwapo kwa harufu mbaya.

Mabaki ya protini mdomoni ambayo huvunjwavunjwa na bakteria na kuwa tindikali ya amino na hapo baadaye inapovunjwa, hutoa gesi yenye harufu mbaya.

Mfano mzuri ni pale protini ijulikanayo kama methionine na cysteine inapovunjwavunjwa kinywani na hivyo kutoa gesi yenye harufu mbaya ijulikanayo kama Hydrogen sulphide.

Mara nyingi harufu ya kinywa inaweza kuwa nzito zaidi baada ya mtu kuamka. Hii ni kwa sababu wakati wa kulala mdomoni kunakuwa na kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni.

Bakteria waliopo mdomoni ni wale wasiohitaji uwepo wa hewa ya oksijeni hivyo kipindi cha usiku tukiwa tumelalala, ndipo huvunjavunja mabaki ya chakula ambayo huambatana na kutolewa gesi zenye harufu mbaya.

Vilevile harufu ya kinywa inaweza kubadilikabadilika kutokana na vyakula tunavyokula ikiwamo vitunguu maji, vitunguu swaumu, hiliki, tangawizi na pia uvutaji sigara na unywaji wa pombe.

Hivyo siyo mara zote kupumua harufu isiyo ya kawaida ni ugonjwa; mara nyingine inakuwa ni tatizo la muda tu lililochangiwa na vyakula na matumizi mengine ya vitu.

Asilimia 10 zilizobaki, mara nyingi husababishwa na matatizo mengine ikiwamo magonjwa ya kooni, puani, shambulizi za nyufa za mifupa iliyopo usoni, magonjwa ya mfumo wa chakula, magonjwa katika mapafu, magonjwa ya masikioni na madhara ya ugonjwa sugu wa mafindofindo.

Vilevile kuwapo kwa majipu ya fizi au meno, vidonda mdomoni au michubuko, vidonda vya kooni na maambukizi ya virusi vya herpes simplex na HPV. Mara chache pia tatizo hili linaweza kuchangiwa na magonjwa ya ini ikiwamo kuharibika kwa ini na majipu katika ini.

Mara nyingine wanaoshtakia tatizo hili hubainika kuwa na tatizo la usafi wa kinywa. Na wanaposhauriwa kuboresha usafi wa kinywa kwa kutumia dawa za meno, au kusukutua na dawa maalumu za kusafisha kinywa nyuma ya ulimi, tatizo huisha haraka.

Tiba ya ugonjwa
Uchunguzi wa tatizo hili huanzia kwa mhusika mwenyewe kueleza historia ya tatizo, kisha wataalamu wa kinywa au daktari wa kawaida humchunguza kwa kumfanyia majaribio na vipimo kadhaa.

Baada ya wataalamu wa afya kubaini ugonjwa ndipo ushauri na matibabu huanza. Kama chanzo cha harufu mbaya ni maradhi ambayo si ya kinywani wataalam watakupa matibabu ya kutibu chanzo hicho.

Kama chanzo cha kutoa pumzi yenye harufu mbaya ni kinywa, wahudumu wa afya watamwelekeza mgonjwa mambo mbalimbali kama ifuatavyo;

Kupiga mswaki katika ulimi mara mbili kwa siku kwa kutumia mswaki laini, kifaa kama kijiko kwa ajili ya kukwangua uso wa ulimi. Pia kutumia dawa yenye kiambata cha kuua bakteria.

Ulaji wa kifungua kinywa chenye afya ikiwamo kula matunda na mboga za majani yenye nyuzi nyuzi, husaidia kusafisha kinywa eneo la nyuma ya ulimi wakati wa kumezwa.

Utafunaji wa bazoka unasaidia kuufanya mdomo usiwe mkavu na hewa ya oksijeni kuingia kinywani kwa wingi. Pia utafunaji wa bazoka unaweza kusaidia kutiririka kwa mate kwa wingi yanayosaidia kusafisha kinywa na kuua vimelea vya maradhi. Mdomo ukiwa mkavu na hautafuni chochote huchangia kujiimarisha kwa bakteria

Kusukutua kwa maji mengi ikiwezekana ya vuguvugu kila mara baada ya kula chakula na kabla ya kwenda kulala. Unaweza pia kutumia dawa maalumu za kusukutulia kinywa zenye dawa ya kuulia vimelea.

Jaribu kuboresha usafi wa kinywa kwa kuusafisha ulimi. Safisha meno kwa mswaki kila unapomaliza kula chakula, ondoa mabaki ya chakula yaliyojibana katika meno na fizi na safisha na sukutua kinywa chako kwa dawa maalumu kabla ya kulala.

Unaweza kutumia vitu asilia kama majani ya minti na karafuu, kama njia ya kupunguza kupumua hewa yenye harufu mbaya.

Ni vyema kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa kila baada ya miezi sita, ili kuweza kubaini magonjwa mbalimbali ya kinywa mapema.
chanzo.Yanayosababisha mdomo kutoa harufu mbaya

Ukitaka Tiba ya kumalizaTatizo lako la kunuka mdomo nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona kabisa.
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.

 
Nenda kwa dentist, unahitaji kusafisha meno na kuelekezwa jinsi ya kusafisha, wengine hapo wanakudanyanya,
Kunuka mdomo inasababishwa na uchafu kwenye sehemu kt ya jino na jino, kuna njia ya kusafisha
Kama yupo Dar aonane na Dr. Lema pale Kairuki Hospital atamfanyia deep cleaning. Amenisaidia sana,na mimi kuna muda ulifika nikadhani hewa inatoka tumboni kumbe sio ni kwenye meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom