Kunuka mdomo kumesababisha niachwe na mpenzi, tafadhali nisaidieni

bishororo

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
254
356
Habari wana jamvi huyu mwanamke toka nimempata hataki nimpige kiss, denda na hata tukiongea huwa anaziba pua.

Sasa jana tumekosana ndo kanambia domo langu linatoa harufu kama choo, nikaishwa mpaka pozi nikakumbuka matukio yote nikiwa na wadau nikiongea tu wanaziba pua.

Dah huu mdomo huu mbona naupiga mswaki kila siku.
 
nunua mdalasini yale magome na asali loweka hayo magome usiku asubuhi chemsha chuja kunywa nusu kikombe ukiwa umechanganya na asali kijiko kimoja nyingine weka kwenye friji jioni kunywa tena usiipashe zoezi liendelee kwa wiki ikiisha unaloweka tena tatizo litaisha, usipende kula vitu vyenye sukari pendelea vichachu
 
Mimi hata nikipata demu mzuri kiasi gani!
Kama ananuka mdomo namuacha!
Wewe jamaa hakuna kitu kinachoaibisha kama harufu ya mdomoni!!Safisha kinywa Vizuri mkuu, at least twice a day!
But it is also good to clean your mouth soon after taking any meal!
 
:D:D:D:D:D:D Mkuu umenikumbusha mbali sanaaaa. Kuna masela tulikuwa tunakwenda club sasa wakiongea na mwanamke maneno mawili tu wanawake hukimbia. Wakaja kuniuliza mbona kila wakiongea na mademu huwakimbia? Sikutaka kuwaambia kama midomo yao inanuka niliweka mkono mfukoni na kuwapa chewing mint gum tu.
 
nunua mdalasini yale magome na asali loweka hayo magome usiku asubuhi chemsha chuja kunywa nusu kikombe ukiwa umechanganya na asali kijiko kimoja nyingine weka kwenye friji jioni kunywa tena usiipashe zoezi liendelee kwa wiki ikiisha unaloweka tena tatizo litaisha, usipende kula vitu vyenye sukari pendelea vichachu
Njia sahii,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupiga mswaki au kusafisha kinywa sio suluhisho. Tatizo liko tumboni. Nenda kamuone daktari akusaidie kutibu matatizo yanayosababisha kunuka mdomo.

Maji lita tano kwa siku inakuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom