Kunuka mdomo kumesababisha niachwe na mpenzi, tafadhali nisaidieni

HAKUNA HARUFU INAKERA KAMA YA MDOMO, BINAFSI HUWA NAUMWA MAFUA YA GHAFLA KAMA NTAPATA HARUFU YA MDOMO, KAMA NI MWANAMKE NTAMCHANA, ASPOELEWA, MTIHANI.

MKUU, JITAHDI UPATE DAWA NZURI YA MENO NA PIA SAFISHA VZUR
 
Habari wana jamvi,

Huyu mwanamke toka nmempata hataki nimpige kiss,denda na hata tukiongea huwa anaziba pua.

Sasa jana tumekosana ndo kanambia domo langu linatoa harufu kama choo nikaishwa mpaka pozi .

Nikakumbuka matukio yote nikiwa na wadau nikiongea tu wanaziba pua.

Dah huu mdomo huu mbona naupga mswaki kila siku au nilikula mavi kipindi niko mtoto?

Tumia kitu inaitwa ''mouth wash'', pia hakikisha pua na koo ni safi yaani ondoa makoozi yote muda wote. Pia sukutua mdomo kila baada ya kula na kunywa chai au uji, pia tumia toothpicks. Usisahau na ulimi kuosha pia. Mwisho sugua meno na kabla ya kulala pia. Baada ya kama wiki mbili mwite huyo mpenzi wako akupime tena.
 
Mkuu,nimewahi kuwa na mshikaji yuko hivo.
Katafute dawa ya meno ya Forever,kitu kama 16,000-18,000.Kuja kumaliza mbili utashangaa,pigia mswaki mara mbili au hata tatu kwa siku.Usisahau mrejesho hapa hapa
 
Tumia kitu inaitwa ''mouth wash'', pia hakikisha pua na koo ni safi yaani ondoa makoozi yote muda wote. Pia sukutua mdomo kila baada ya kula na kunywa chai au uji, pia tumia toothpicks. Usisahau na ulimi kuosha pia. Mwisho sugua meno na kabla ya kulala pia. Baada ya kama wiki mbili mwite huyo mpenzi wako akupime tena.
Hili la kumeza makohozi inaweza ikawa sababu rafiki yangu atemi anameza hata akiwa sehemu inaruhusu kutema hatemi anameza basi domo linanuka kama chemba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee. Na wanaume wakinuka mdogo wananuka haswaaa.

Nilikutana na mtu hivi majuzi mahali pangu pa kazi nilijuta kuongea nae kwa jinsi alivyokuwa ananuka mdomo.

Ila kwa baadhi ya wanaume kwao limeshakuwa jambo la kawaida.
 
Unywaji wa maji kila mara pia hupunguza harufu kinywani. Piga mswaki kila baada ya mlo. Usilale bila kupiga mswaki. Sugua ulimi na sukutua kwa maji mengi. Tafuna bubble gum. Ikishindikana kamuone daktari meno akufanyie usafi wa kinywa
 
Habari wana jamvi,

Huyu mwanamke toka nmempata hataki nimpige kiss,denda na hata tukiongea huwa anaziba pua.

Sasa jana tumekosana ndo kanambia domo langu linatoa harufu kama choo nikaishwa mpaka pozi .

Nikakumbuka matukio yote nikiwa na wadau nikiongea tu wanaziba pua.

Dah huu mdomo huu mbona naupga mswaki kila siku
Kula matango pia yanakata harufu ya domo
 
:D:D:D:D:D:D Mkuu umenikumbusha mbali sanaaaa. Kuna masela tulikuwa tunakwenda club sasa wakiongea na mwanamke maneno mawili tu wanawake hukimbia. Wakaja kuniuliza mbona kila wakiongea na mademu huwakimbia? Sikutaka kuwaambia kama midomo yao inanuka niliweka mkono mfukoni na kuwapa chewing mint gum tu.
mkuu na wewe ulikuaga na tatzo hilo?
 
Kuna dawa za kusukutua znauzwa pharmacy kaulzie, kupga mswaki tuu haitoshi inaezekana unatatzo

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaa katika vitu vigumu kuvumilia ktk mapenzi mojawapo ni hilo kunuka mdomo, soksi, kwapa la beberu duu mimi siwezi kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom